LIGI DARAJA LA KWANZA CHANETA CUP KUHITIMISHWA KESHO UWANJA WA SOKOINE, MULUGO KUWA MGENI RASMI.


Mwenyekiti wa Chama cha Netboli Taifa(CHANETA) Annah Kibira anawaomba wapenzi wa mpira huo Mkoa wa Mbeya kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Sokoine kwa sherehe za kufunga ligi hiyo.
Mwenyekiti wa Chaneta Mkoa wa Mbeya, Mary Mng’ong’o amesema Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo Philipo Mulugo ambaye atashuhudia michezo miwili na kugawa zawadi kwa washindi.
Viongozi wa chaneta wakiongea na waandishi wa habari

Mwenyekiti wa Chama cha Netboli Taifa(CHANETA) Annah Kibira anawaomba wapenzi wa mpira huo Mkoa wa Mbeya kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Sokoine kwa sherehe za kufunga ligi hiyo.
Kibira amesema ligi hiyo itahitimishwa kwa michezi miwili ambayo ni kati ya Hamambe dhidi ya Jeshi Staa na mchezo mwingine kati ya Filbert Bayi dhidi ya JKT Mweni.
Amesema katika michezo hiyo mgeni rasmi ambaye anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo atashuhudia michezo hiyo kwa kuzikakugua timu hizo kabla ya kutoa zawadi kwa washindi na kufunga.
Hata hivyo Kibira ametoa wito kwa wadau wa michezo nchini kujitokeza kudhamini ligi hiyo ili kuwa na mvuto kama michezo mingine ili kuzifanya timu shiriki kuwa nyingi.
Kibira amesema kukosekana kwa wafadhili wa Ligi za Netboli kumechangia timu kupungua katika Ligi daraja la Kwanza mwaka huu ambapo kwa kawaida zilitakiwa kuwa na timu 20 lakini hadi ligi inafunguliwa Agosti 24, Mwaka huu jumla ya timu 12 zilijitokeza na kushiriki ligi hiyo itakayohitimishwa Septemba Mosi, Mwaka huu.
Alisema kutokana na kushiriki kwa timu chache jumla ya michezo 66 ikakuwa imefanyika kufikia kesho kwa amani, Upendo na Mshikamano ukihusisha timu 12 na kuongeza kuwa kwa mujibu wa Kanuni za Chaneta timu nane ambazo zilishindwa kushiriki zinatakiwa kushuka daraja hivyo hatima yao Kamati tendaji itaamua.
Akizungumzia kilele cha kuhitimisha Ligi hiyo Mwenyekiti wa Chaneta Mkoa wa Mbeya, Mary Mng’ong’o amesema Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo Philipo Mulugo ambaye atashuhudia michezo miwili na kugawa zawadi kwa washindi.
Mng’ong’o amesema undeshaji wa ligi hiyo umekutana na changamoto nyingi lakini kubwa kabisa ni ukosefu wa fedha uliotokana na uchangiaji duni wa wadau hali iliyopelekea timu kujigharamia zenyewe.
Aidha ametaja msimamo wa ligi hiyo kuwa inaongozwa na timu ya JKT Mbweni yenye alama 20 sambamba na timu ya Filbert Bayi yenye alama 20 lakini ikiwa na magoli machache dhidi ya JKT Mbweni.
Timu ya Magereza Morogoro inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 17 ikifuatiwa na Jeshi Staa yenye alama 15 na timu mwenyeji ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya (HAMAMBE) ikishika nafasi ya tano kwa alama 13 huku timu ya Polisi Mbeya ikifunga mkia kwa alama 2 sambamba na CMTU kutoka Dar Es Salaam ikiwa haina alama hata moja.

Na Mbeya yetu

Post a Comment

0 Comments