Redd’s
Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa (19) akipozi kwa
picha Mara baada ya kuibuka mshindi wa taji hilo na kuwa mrembo wa
kwanza kutinga nusu fainali za Miss Tanzania 2013 baada ya kuwashinda
warembo wenzake 29 katika shindano hilo dogo kuelekea fainali za Redd’s
Miss Tanzania 2013.
Mrembo Happiness Watimanywa akiwa amekubwa na butwaa baada ya kutajwa Mshindi wa Redd's Miss Photogenic 2013.
Redd’s
Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa (katikati) akipozi
kwa picha na warembo wengine walioingia hatua ya tano bora ya kumsaka
mshindi wa taji la Miss Photogenic 2013. Kutoka kulia ni Anastazia
Donald ,Latifa Mohamed, Clara Bayo na Jacline Luvanda.(
Warembo
wengine Walioshiriki shindano hilo wakifuatilia utangazwaji wa matokeo
hayo katika Hoteli ya Giraffe Ocean View katika kambi yao.
******** ********
Mrembo wa Mkoa wa Dodoma, na
mwakilishi wa Kanda ya Kati, Happiness Watimanywa, juzi amenyakua taji
la Redds Miss Tanzania Photogenic 2013 na kuwa mrembo wa kwanza kuingia
hatua ya nusu fainali ya shindano la Redds Miss Tanzania 2013.
Happiness amefanikiwa kuingia hatua hiyo ambayo itaingiza warembo 15 bora na kuwashinda warembo wenzake 29 ambao wapo katika kambi ya Redds Miss Tanzania 2013.
Shindano hilo dogo la Haiba ya Picha “Miss Photogenic”
alipatikana baada ya jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha
mashuhuri nchini Tanzania wakiongozwa na Jaji Mkuu Mroki Mroki kutoka
magazeti ya SerIkali Daily News, Habarileo na Spotileo.
Mapema
akitaja majina ya warembo walioingia hatua ya tano bora Mroki aliwataja
majaji wengine aliyoshirikiana nao kuwa ni Mpigapicha wa Jambo Leo
Richard Mwaikenda na Mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Aika Kimaro.
Dalili
za kuonesha kuwa Happiness amekubalika hata kwa washiriki wenzake
katika shindano hilo ziliibuka wakati Mroki akitaja majina ya warembo
waliofanikiwa kuingia hatua hiyo na lilipotajwa jina lake ukumbi wa
Emanyata uliofurika wakazi wa mji wa Monduli na warembo ulilipuka kwa
kwashangwe.
Warembo
watano walifanikiwa kuingia katika mchujo huo ni pamoja na Anastazia
Donald ,Latifa Mohamed, Clara Bayo na Jacline Luvanda na Happiness
Watimanywa aliyeibuka mshindi.
Warembo
wa Redds Miss Tanzania watashindana tena katika shindano la Miss Top
Model linalotaraji kufanyika Septemba 7 mwaka huu, katika Hotel ya Naura
Spring jijini Arusha.
Mataji mengine yatakayo waniwa na warembo hao na
washindi kuingia moja kwa moja klatika hatua ya Nusu fainali ni Miss
Talent, Miss Personality na Miss Sports Woman. Taji la Miss Photogenic
lilikuwa linashikiliwa na mrembo Lucy Stephano kutoka Manyara na Kanda
ya Kaskazini, kutoka Shinyanga na Kanda ya Ziwa.
Fainali za mwaka huu za Redds Miss
Tanzania zinataraji kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar
es Salaam Septemba 21,2013.
0 Comments