Na Bryceson Mathias
HIVI
karibuni Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mtwara ilimfutia shtaka la
kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM)
Hasnein Murji (46) aliyepandishwa kizimbani Juni 10, mwaka huu na
kufunguliwa kesi ya uchochezi.
Hatua
hiyo ilikuja baada ya Wakili wa utetezi, Peter Kibatala kuiomba
mahakama kuifuta kesi hiyo iliposomwa Julai 3, mwaka huu kwa madai hati
ya mashtaka ni dhaifu kisheria na haionyeshi ni makosa yapi mtuhumiwa
aliyatenda.
Kibatala
aliieleza mahakama kuwa kifungu cha 129 na 132 cha sheria ya mwenendo
wa makosa ya jinai ni lazima mshtakiwa aelezwe mashtaka yake wazi wazi
yanayomkabili, jambo linalopelekea baadhi ya wanasiasa wahoji
akumulikaye mchana usiku atakuchoma?
Murji
alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani akikabiliwa na kesi ya
uchochezi anayodaiwa kuifanya Januari 19,mwaka huu katika eneo la Ligula
mkoani humo Mtwara.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi Dynes Lyimo alifuta shtaka hilo na kumwachia mshtakiwa
huru baada ya kesi hiyo kuahirishwa tangu Julai 3, mwaka huu.
Miongoni
mwa waliohusishwa na kesi hiyo ni viongozi wa upinzani Katani Ahmed
(33) na Saidi Kulaga (45) wa CUF waliokabiliwa na mashtaka matatu ya
kula njama, kufanya uchochezi na kuamsha hisia mbaya kwa wakazi wa
Jamhuri.
Murji
alikabiliwa na tuhuma za uchochezi wa vurugu za kupinga kujengwa bomba
la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi jijini Dar es Salaam,
zilizosababisha vifo vya watu watatu na wengine kadhaa kujeruhiwa Mei,
2013.
ni rai yetu kufahamu kama Mahakama imemfutia mashitaka Murji,
Waliomshitaki wamemuonea? Mbali ya kumuonea, Murji na wananchi wake
wanakitazamaje CCM ambacho Serikali yake iliyomsimamisha awawakilishe na
imeshamdharirisha hivyo pa sina ukweli?
Katika utetezi wake, Kibatala aliiomba mahakama imfutie mteja wake
mashtaka kwa madai, hati ya mashtaka iliyowasilishwa mahakamani ilikuwa
na upungufu mkubwa wa kisheria.
Alidai miongoni mwa upungufu uliokuwamo kwenye hati, ni pamoja na
kutokuwa na maelezo yanayoonesha kosa alilokuwa akishtakiwa mteja wake.
Alidai
vifungu namba 129 na 132 vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai
namba 20 kama ilivyorejewa na marejeo ya 2002, vinataka hati za mashtaka
zizingatie na kutekeleza suala hilo.
Kwa mujibu wa Kibatala, kinyume cha hivyo, vifungu hivyo vinaipa
mahakama uwezo wa kufuta hati ya mashtaka yenye upungufu wa kisheria.
Murji alisomewa mashtaka na Mwanasheria wa Serikali, Kisheni Mtalemwa
akisaidiana na Zuberi Mkakatu, na kudaiwa Januari 19, 2013 katika maeneo
ya Ligula Mtwara alichochea watu wafanye vurugu kinyume cha sheria.
Katika kesi hiyo, pia kulikuwa na washitakiwa 91 walioshitakiwa, na
baadhi waliachiwa kwa dhamana na wengine walipelekwa rumande baada ya
kushindwa kutimiza masharti.
Murji pia alirudishwa rumande baada ya kukana mashitaka na kushindwa
kutimiza masharti ya dhamana awasilishe mahakamani hati ya kusafiria,
mdhamini mwenye mali isiyohamishika, yenye thamani isiyopungua Mil.20/-
na ifanyiwa tathmini.
Pia
alitakiwa asifanye mikutano ya hadhara bila kibali cha Polisi wa Mkoa,
na kutokana na Murji kutokuwa na pasi yake ya kusafiria siku hiyo papo
hapo ilishindikana.
Je
alivyofanyiwa Murji na Serikali ya Chama chake, bado atakuwa na nguvu
ya kuwatetea wananchi wake? Lakini wanajifunza nini katika hali kama
hii? Tusiamshe hasira za wananchi bila sababu.
nyeregete@yahoo.co.uk 0715933308
0 Comments