Add caption
LIGI ya Mpira wa pete (CHANETA CUP) inayofanyika
Kitaifa katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Mkoani Mbeya imeanza kwa kasi
baada ya timu nane kutoana jasho katika Mechi za ufunguzi.
Mechi nne za ufunguzi zililazimika kufanyika
Asubuhi kutokana na kufunguliwa kwa pazia la Ligi kuu la mpira wa Miguu kati ya
timu ya Kagera Sugar na Mbeya City katika uwanja huo huo hivyo kupisha
muingiliano wa Ratiba.
Katika mchezo wa kwanza ulizikutanisha timu za
Polisi Mbeya iliyomenyana vikali na timu ya Tumbaku kutoka Mkoani Morogoro
ambapo Timu ya Tumbaku iliibuka kidedea kwa magoli 35 dhidi ya 17 waliyoyapata
timu ya Polisi Mbeya.
Mchezo uliofuata ulikuwa kati ya timu ya Jeshi
la Uhamiaji kutoka Dar Es Salaam dhidi ya Polisi Arusha na matokeo kuishia kwa
Uhamiaji kuibuka na ushindi wa Magoli 27 kwa magoli 19 ya timu ya Polisi ya
Arusha.
Timu za Polisi zilizidi kumwagiwa magoli katika
Mchezo wa Tatu uliozikutanisha timu ya Polisi Mwanza dhidi ya Timu ya Filbert
Bayi ya Dar Es Salaam ambapo timu ya Polisi ililala kwa magoli 21 dhidi ya
magoli 33 ya Filbert Bayi.
Timu ya Magereza kutoka Mkoani Morogoro pia
ilichachafya timu ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya maarufu kama Hamambe katika
mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa kutokana na ufundi wa wafungaji wa pande
zote mbili ambapo hadi kipenga cha mwisho cha mchezo huo Hamambe magoli 28 na
Magereza 31.
Na Mbeya yetu
|
0 Comments