Na Elizabeth John
BAADA ya kufanya vizuri na kazi yake ya ‘Kimbiji’, msanii wa
muziki wa kizazi kipya nchini, Rahim Rummy ‘Bob Junior’, anajipanga kuisambaza
kazi yake mpya hivi karibuni.
Mbali na Kimbiji, mkali huyo alishawahi kutamba na ngoma
zake kama ‘Nichuum’, ‘Oyoyo’ na nyinginezo,
ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Bob
Junior alisema yuko katika maandalizi ya kuisambaza kazi hiyo ambayo hajataka
kuitaja jina.
“Unapotaja jina kabla haujasambaza, kuna baadhi ya watu
wanakuwa wanachukua mawazo yako na unapoisambaza yako, kinakuwa sio kitu kipya,
hivyo nitakapoisambaza kila mmoja ataijua jina,” alisema msanii huyo ambaye pia
ni mtayarishaji wa muziki huo.
Alisema kazi hiyo ataisambaza pamoja na video yake kwa lengo
la kuwapa radha kamili mashabiki wake.
0 Comments