Mkurugenzi
wa Taasisi ya AMREF Tanzania Dk.Festus Ilako akiongea na waandishi wa
Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu halfa ya chakula cha hisani ya
kuchangisha fedha itakayokuwa na kauli mbiu ya “Stand for
African(Tanzania) Mother’s ili kuchangia mfuko wa kuwasaidia wakina mama
na watoto,halfa hiyo itafanyika Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Montage
Bi.Teddy Mapunda na kulia ni Naibu Mkurugenzi wa AMREF Tanzania Dk,
Rita Noronha. Mkurugenzi
Mtendaji wa Montage Bi.Teddy Mapunda akifafanua jambo kwa waandishi wa
Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu halfa ya chakula cha hisani ya
kuchangisha fedha itakayokuwa na kauli mbiu ya “Stand for
African(Tanzania) Mother’s ili kuchangia mfuko wa kuwasaidia wakina mama
na watoto,halfa hiyo imeandaliwa na AMREF wakishirikiana na Montage
itafanyika Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam.
Waandishi
wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya AMREF Tanzania
Dk.Festus Ilako leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea
nao kuhusu halfa ya chakula cha hisani ya kuchangisha fedha
itakayokuwa na kauli mbiu ya “Stand for African(Tanzania) Mother’s ili
kuchangia mfuko wa kuwasaidia wakina mama na watoto,halfa hiyo
itafanyika Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.(Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo)
Mkurugenzi wa Taasisi ya AMREF Tanzania Dk.Festus Ilako akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Bi.Teddy Mapunda pamoja na maafisa wengine wa AMREF mara baada ya mkutano kumalizika Mkurugenzi
Mtendaji wa Montage Bi.Teddy Mapunda akiwa naEliminatha Pascal Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano AMREF kulia wakionyesha ujumbe uliopo katika
bango kuhusu hafla hiyo ya kuchangia mafunzo ya wakunga.
Eleuteri Mangi-Maelezo
TAASISI
ya AMREF Tanzania imetangaza inatayarisha chakula cha hisani
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kuwasaidia akina mama
na watoto itakayokuwa na kauli mbiu “Satand for African mothers“ mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.Jakaya Kikwete.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa AMREF Tanzania Dr. Festus Ilako
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
“Fedha
zitakazochangiwa zitakuwa kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kuwasaidia
akina mama na watoto ili kupunguza vifo vya wanawake na watoto” alisema
Dr.Ilako.
Dr.
Ilako alisema kuwa hafla hiyo itafanyika Oktoba 11, 2013 katika hoteli
ya Serena jijini Dar es salaam ambapo taasisi yake inashirikiana na
Serikali ya Tanzania katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya Milenia
ya kuboresha huduma za afya hasa za akina mama na watoto.
Dr.
Ilako alisema “ili kufikia malengo hayo, kunahitajika kuwa na wakunga
wa kutosha kuimarsha Nyanja ya uzazi salama kufanikisha malengo ya
millennia”.
Dr.
Ilako alitoa wito kwa taasisi mbalimbali kujitokeza siku hiyo na
kujitolea katika kuchangisha fedha ili kufikia malengo ya ya kutoa elimu
kwa wakunga 3,800 ifikapo 2015. Tangu kampeni hiyo ianzishwe tayari wakunga 10 wamewezeshwa kupata elimu na wengine 70 wategemewa kujiunga.
Ili
kufanikisha malengo kuboresha huduma ya mama na motto kunahitajika
uboreshaji wa ujuzi wa wakunga 2800 kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya
“e-lerning “na kutoa mafunzoya awali kwa walau wakunga 1000 mpaka mwaka
2015.
Mkurugenzi
huyo aliitaja mikoa inyonufaika na mpango huo ni mpaka sasa ni Tanga,
Mtwara na Simiyu na kuainisha kuwa lengo la taasisi yake ni kiifikia
mikoa yote ya Tanzania.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Tanzania Teddy Mapunda
alisema kuwa wanatarajiwa kuhudhuria ni pamoja na viongozi wakuu wa
taasisi mbalimbali za kiserikali, za binafsi ndani na nje ya nchi na
wananchi wote. Mapunda pia aliwaomba
vyombo vya habari kuwa mabalozi wazuri ili watanzania wajue AMREF
inafanya nini ili watanzania waweze kuwa na uzazi salama.
Kufanikisha
azma hiyo Mapunda aliwaomba watu wote wenye mapenzi mema kutoa
michango yao na kuisilisha kupitia huduma ya M-pesa kwa namba
0752-167286, au akaunti ya NBC makao makuu, 0111030004548 ama kununua
meza ya watukumi katika hafla hiyo kwa kiasi cha dola 1500 sawa na
shilingi 2430000 za kitanzania.
Kampeni
ya “Stand up for African Mothers” ilizinduliwa mwaka 2012 ambapo AMREF
ina zaidi ya miaka 57 katika kutoa huduma za kijamii sehemu mbalimbali.
Wadhamini wa hafla ya kuchangisha fedha hiyo ni banki ya AMREF ikishirikiana na benki ya NBC, Serengeti Breweries na ITV.
0 Comments