Wladimir Klitschko BONDIA ASIE NA MPINZANI UZITO WA JUU




Wladimir Klitschko

Bondia mbabe uzito wa juu duniani



KWA wakati huu Wladimir Klitschko ni jina maarufu zaidi katika ulimwengu wa ngumi za kulipwa kutokana nna kuwa na rekodi nzuri ya kutopigwa.


Kutokana na mchezo wa bondia huyo amejikusanyia fedha nyingine na kuweza kuishi maisha ya kifahari nchini Ujerumani.


Anakadiriwa kuwa na utajiri unafikia dola milioni 30.


Klitschko kwa sasa  ana mikanda minne ya ubingwa wa uzito wa juu duniani.


Ni bondi ambaye anaweza kuzungumza lugha nne za Kingereza, Ukraine, Kijerumani na Kirusi.


Kwa sasa mbabe huyo anamiliki mikanda ya ubingwa wa IBF, IBO na WBO akiwa ameshinda mfululizo mapambano 15.


Anatajwa kuwa ni bondia nne aliyetetea na kukaa na mataji kwa muda mrefu zaidi kwa wakati wote,

 Klitschko ameweza kutetea  ubingwa wake mara 14.

Joe Louis na Larry Holmes ni mabingwa wengine wa uzito wa juu waliowahi kutetea ubingwa wao mara nyingi.


Kwa upande mwingi, Wladimir  na kaka yake Vitali ambaye ni bingwa wa uzito wa juu duniani wa

WBC  wanachukuliwa kuwa ni wanadugu wa kwanza kuweza kutwaa mataji ya ubingwa wa dunia kwa wakati mmoja. KBoxrec  imewataja Klitschko kwa kuwa bingwa wa tatu kwa kupigana bila ya kurudi nyuma Desemba 2012.

Aliwahi kuchukuliwa na katika klabu ya Gwardia Warszawa  akiwa kama kocha wao mkuu.


1993,  maisha yake yalibadilika wakati alipotajwa kuwa ni Bingwa wa uzito wa juu wa Ulaya kwa vijana.


Baadaye, aliitwa “The Steel Hammer” Nyundo ya chuma au “Dr. Steel Hammer” kwa kiswahili Dk Nyundo.


Dunia ilimfahamu na akafahamika zaidi baada ya kuibuka na ushindi katika pambano lake dhidi ya Paea Wolfgramm katika mashindano ya olimpiki 1996. Miaka minne baadaye, alianza kucheza ngumi za kulipwa.


Mapambano yake ya kukumbukwa ni pamoja na dhidi ya Chris Byrd, Sultan Ibragimov, Samuel Peter, Eddie Chambers  na dhidi ya David Haye.


Katika mapambano 62, alishinda 59 na kupoteza 3. Katika ya mapambano 59  aliyoshinda, 50 alishinda kwa knockout.


Kwa sasa mpambe huyo hana mashara anapokuwa ulingoni, haipaswi kufanya mashihara kwa kuwa anaweza kukutwanga kwa ngumi moja tu. Henu jaribu kufikiria ana nguvu kiasi gani  katika ngumi zake.


Kutoka kutokuwa na kitu hadi kuwa na kila kitu


Anasema anaweza kupigana kwa raundi 12 bila ya matatizo na kufurahia kupigana.Anafurahia kupigana. Anasema kuwa urefu unamsaidia na amekuwa akiutumia.


Anasema mabondia wafupi wana mikono mifupi na miguu mifupi lakini wana kasi . Watu warefu wana faida ambapo kila mmoja hujaribu kuutumia.


Anasema kila wakati katika maisha amekuwa na malengo ya kushinda pambano.


"Nina malengo yangu katika maisha, kuwa bingwa wa michezo, ni muhimu sana kushinda kwa sababu, kwa sasa, ninataka kuwa namba moja katika IBF na WBO."


Anasema katika ngumi ni muhimu kuwa na stamina vinginevyo bondia ni rahisi kupigwa au hata kufa.


Anasema kuwa kukosolewa ni changamoto kwake.  Anasema kushindwa si kitu ambacho anakitaka katika uchezaji wake.


Yeye na kaka ya, Vitali ni watoto wa aliyekuwa rubani wa helikopta katika uliokua Umoja wa Nchi za Kisovieti.


Wladimir Klitschko ni mtu maarufu Ulaya, aliigia miakataba na kampuni za Mercedes-Benz, Warsteiner, McFit na Strellson ambayo imempatia fedha nyingi.


Vitu anavyopenda


Kupigana ngumi


Anapenda kwenda katika ufukwe wa Florida  wakati wa mapumziko.


Anapanda kwenda  ufukwe wa Miami  na anapenda kwenda mapumziko

Italia


Kutokana na kuwa na fedha amekuwa akitoa misaada kwa taasisi za kusaidia jamii ikiwemo ya

Laureus Sport for Good.

Mfuko huo umelenga kusaidia watu kujiingiza kwenye michezo, kuhamasisha watu kupata mafanikio, kushinda maovu na kufurahia mafanikio.


Pia ni balozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni akishughulika  na kuhamasisha uhusiano wa kimataifa katika masuala ya kusaidia elimu, sayansi, utamaduni na mawasiliano.


Wladimir Klitschko anapenda kutumia vifaa vya 1A Few anapokuwa ulingoni.



Jina: Wladimir Klitschko

Alizaliwa Machi 25,1976

Mahari: Ukraine
Aliona na kutaliki
Kazi yake:
Bingwa wa ngumi wa uzito wa juu

Post a Comment

0 Comments