Na
Elizabeth John
WASANII
wa Tanzania wameshauriwa kufuata maadili ya nchi katika video za nyimbo zao ili
wasipoteze sifa ya nchi katika vizazi vijavyo.
Baadhi
ya wasanii wamekua wanawatumia wakinadada mbalimbali kwaajili ya kupendezesha
video hizo huku wakivaa nguo za ajabu ambazo kiukweli kiutamaduni haipendezi.
Kauli
hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaaam hivi karibuni na msanii anayeibukia katika
fani ya muziki wa hip hop nchini, Emmanuel Peter Sahani ‘Plate’ ambapo alisema
baadhi ya video za Tanzania
zinaidhalilisha nchi yetu.
“Kiukweli
haipendezi hata kidogo video zingine huwezi kuangalia mbele za wazazi wako
maana mambo yanayooneshwa humo yanatisha, tunawaharibu watoto ambao kila wakati
hupenda kuangalia video za wasanii wa bongo, kazi ya msanii ni kuelimisha jamii
na sio kupotosha,” alisema.
Alisema
utandawazi ndio unaharibu maisha ya vijana wa Tanzania, maana kila kijaan
ambaye ataangalia jinsi nchi za wenzetu wanavyovaa nae atataka ajaribu yeye
atatokaje.
0 Comments