SUPER D |
BENDI Kongwe ya Mziki wa dansi nchini
Msondo Ngoma imeingia Studio kurekodi nyimbo zake mpya zitakazokuwa
katika Albam moja akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa Bendi
Hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa bendi yake kwa sasa imeingia
studio kukamilisha kurekodi nyimbo zao mpya
Alizitaja nyimbo hizo kuwa li Suluhu
uliotungwa na Shabani Dede,Lipi Jema na Baba Kibebe wa Eddo
Sanga,Nadhili ya mapenzi wa Juma Katundu,Kwa momba akuna Uridhi
,Machimbo nyimbo zote hizo zikikamilika zitawekwa kwenye albam moja kwa
ajili ya kuwapa raha mashabiki wao wawapo majumbani
Super D aliongeza kuwa bendi hiyo kwa
sasa imesimamisha maonesho yake lakini watakapoanza sikukuu ya Idi mosi
watatoa burudani katika ukumbi wa DDC Kariakoo idi pili watakua TTC
Chang'ombe na idi tatu watavuka bahari kuelekea visiwa vya karafuu na
kufanya onesho lao Zanzibar
Bondi hiyo kwa sasa inatamba na nyimbo zake mbalimbali wameweka nia ya kukonga mashabiki wa bendi hiyo kwa kupiga nyimbo mpya na zazamani ili kila mtu apate burudani unajua bendi yetu kongwe lazima tutoe burudani za aina tofauta aliongeza Super D
Bendi hiyo iliyopata umarufu mkubwa
miaka ya nyuma imewahakikishia wapenzi wake kurudi katika ubora ule ule
kama ilivyokuwa awari
0 Comments