Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Joto Hasira’
mwanadada ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya
nchini, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa
jina la ‘Yahaya’ katika vitio mbalimbali vya redio.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Jay Dee alisema
anaomba sapoti kwa mashabiki wake na anaimani itafanya vizuri kutokana na ubora
wa mashairi ambayo yametumika katika wimbo huo.
“Naomba mashabiki wangu waipokee vizuri kazi hii
naimani itafanya vizuri, mbali na hiyo nipo katika hatua za mwisho za uandaaji
wa video ya ngoma hiyo, mashabiki wakae mkao wa kula,” alisema Jide.
Jide
alishawahi kutamba na ngoma zake zingine kama, Natamani Kuwa malaika,
Single Girl na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri
katika tasnia ya muziki huo.
0 Comments