Warembo
wa Redds Miss Kinondoni 2013 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani), kwa sasa
warembo hao wameshaingia katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es
Salaam kujinoa kwa ajili ya Redd's Miss Kinondoni Talent 2013
zinazofanyikia ukumbi wa Shekinah Garden Mbezi Beach na Fainali
zinafanyika Juni 21 ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip.
---
Na Cathbert Angelo, Kajunason Blog.
SHINDANO la
Redd’S Miss Kinondoni Talent 2013 linatarajiwa kufanyika alhamisi ya
Juni 25 katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es
Salaam ambalo litashirikisha warembo wapatao kumi na mbili ambao
watachuana kumpata mrembo mwenye kipaji.
Akizungumza
mratibu wa shindano hilo, Dennis Ssebo alisema maandalizi ya kuelekea
shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza mshindi atakabidhiwa zawadi
zake kwenye fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Juni 21 mwaka
huu katika uwanja wa hoteli ya Golden Tulip.
“Ninachoweza
kusema shindano la mwaka huu litakuwa la aina yake kutokana na kusheheni
warembo bomba wenye mvuto na hivyo kuonyesha kutakuwa na mchuano mkali
miongoni mwao “Alisema Ssebo.
Warembo warembo
wanaotarajiwa kumenyana ni kutoka katika vitongoji vya Sinza, Ubungo na
Dar Indian Ocean ambao kwa pamoja wanaunda Redd's Miss Kinondoni 2013.
Alisema kwamba
shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya
Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki
wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.
Mashindano ya
Redd's Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy
Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte
Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog,
Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com,
JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog,
Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.
0 Comments