Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR), Moses Machali akiwa amelazwa wodini. |
Akisiendelea kupata nafuu baada kushambuliwa.
|
Kamanda
wa Polisi mkoani Dodoma,David Misime akizungumza na waandishi wa habari
mjini humo jana kuhusu tukio la Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR) Moses
Machali kuvamiwa na vibaka eneo la Area E juzi usiku.
Na. Jeshi la Polisi Dodoma.
DODOMA IJUMAA JUNI 21,
2013. Jeshi la Polisi Mkoa Dodoma linawashikilia watu
wawili kwa tuhuma za kumvamia na kumshambulia Mheshimiwa MOSES S/O MACHALI,
miaka 31, Muha, Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia NCCR – Mageuzi wakati anaelekea
nyumbani kwake
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. David.
A. Misime alisema Tukio
hilo limetokea tarehe 20/06/2013 majira ya 19.00 hrs katika eneo la Area ‘E’ katika Manispaa ya
Dodoma
“alikutana
na vijana wanne (4) walikouwa amesimama katikati ya barabara akapiga honi
lakini hawakupisha. Aliamua kuwauliza “Jamani mnasimama katikati ya barabara si
nitawagonga?” Nao wakamjibu: “Wewe si unajifanya mtto wa Mbunge, tutakupiga
sasa”.
Alisisitiza
Kamanda Misime
Kamanda Misime alisema Mheshimiwa
alipojaribu
kupita vijana hao walipiga gari lake. kitu ambacho kilimfanya ashuke ili atazame kama gari hilo limepata
uharibifu.wowote, ndipo vijana hao wakaanza kumshambulia kwa ngumi na mateke
huku naye akijitahidi kujihami.
Hata hivyo Bw.Misime
alisema, walitokea vijana wawili (2) na
kumsaidia. Mheshimiwa mbunge ambapo kijana mmoja kati ya waliokuwa
wanamshambulia Mheshimiwa Machali ‘alimng’ata’ mgongoni kijana aliyekuwa
anamsaidia Mheshimiwa Mbunge.
Bw. Misime alisema
Watuhumiwa baada ya kuona wamezidiwa nguvu walitimua mbio. Ambapo pia
Mheshimiwa Machali aligundua kuwa simu yake ya mkononi wameondoka nayo vijana
hao.
Kamanda David. A. Misime
alisema jeshi la Polisi mkoani Dodoma lilifanya Msako mkali ulifanyika usiku wa manane ambapo watuhumiwa wawili (2)
walikamatwa ambao aliwataja kuwa ni JEREMIA LAWRENT MKUDE@ JERRY, Miaka 18, Mkaguru Mkazi
wa Chaduru, Manispaa ya Dodoma. aliyekutwa akiwa na jeraha usoni alilopata
wakati anapambana na Mheshimiwa Mbunge na vijana waliokuwa wanamsaidia.
Kamanda huyo wa Polisi Mkoa
wa Dododoma alimtaja mtuhumiwa mwingine anayeshikiliwa na jeshi la polisi
kuwa ni CHARLES CHIKUMBILI, Miaka 22, Mkulima, Mkazi wa Swaswa,
katika Manispaa ya Dodoma.
Kamishna
Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Bw. David
Misime alisema askari walipowafanyia
upekuzi wa mwili watuhumiwa usiku huo wa manane wamekutwa na
misokoto miwili (2) ya bhangi.
MWISHO:
CONTACT:
POLISI MKOA WA DODOMA
DAWATI LA HABARI, ELIMU NA MAHUSIANO,
Phone: 0715 006523, Luppy Kung’alo – Mrakibu
msaidizi wa Polisi (ASP)
|
0 Comments