Nexus onsultancy Agency CEO Bobby Bharwani . Rockstar 4000 Head of Talent and New Business Christine Mosha 'Seven'.
Wasanii wa kundi la Orijino Komedi katika picha ya pamoja na Wadau wao.
Kundi la kipaji cha televisheni“OrijinoKomedi”
linaloongoza nchini kwa vipindi vyake kupitia television imeingia mkataba na kampuni
ya Nexus Consulting Agency kwa kushirikiana na Rockstar 4000. Mkatabahuuunakuwawa
kwanza kwa wasanii wa luninga kupitia kampuni hii ya Nexus.
Nexus imenunua haki zote za usimamizi
wa biashara na uongozi wa kundi hilo ambalo linajulikana sana nchini kupitia vichekesho
vyake kupitia vituo vya televisheni na matamasha mbalimbali ambapo mkataba huu utakuwani
kwa ajili ya kusimamia kipindi hiki cha vichekesho kinachoundwa na wachekeshaji
saba wajulikanao kama; Joti, Maclegan, Masanja, Wakuvanga, Mpoki, Venguna David
Seki ambacho kimekuwepo hewani kwa mfululizo wa miaka sita.
Kushirikiana na Orijino Komedi
ni kitu cha muhimu kwa Nexus kwani siku zote imekuwa ikitamani kufanyakazi kwa karibu
na kundi hilo na kuthamini kazi zao kutokana na vipaji vya hali ya juu walivyokuwa
wakionyesha wasanii wa kundi hilo; alisema Mkurugenzi mkuu wa Nexus, Bwana
Bobby Bharwani.
“Nimefurahishwa sana kufanya kazi na
watu wenye vipaji vya hali ya juu na kuiingia mkataba na Kampuni ya Nexus
Agency. Kwa pamoja tumedhamiria kukuza na kubadilisha dhama ya vipaji na sanaa kutoka
ilipo na kuwa ya kimataifa” alisema Christine “Seven” Mosha,Mkuuwakitengo cha
Vipajina Uendelezaji wa Biashara kutoka ROCKSTAR4000.
Muandaji wa vipindi vya Orijino Komedi,
Sekioni Davis ‘Seki’ amesema wana furaha kuingia mkataba wakazi na kampuni
ya Nexus Agency naRockstar 4000 Africa, ambapo ameahidi kufanyakazi kwa bidii kuhakikisha
wanafikia malengo yao ya kukidhi haja ya soko.
Kwa kushirikiana na Rockstar 4000,
nexus inatambua na kuthamini vipaji hivyo itahakikisha inaendeleza vipaji vya wasanii
wa kundi hilo ilivipaji vyao viweze kufikia kiwango cha juu vya ufanisi ndani ya
Afrika na kimataifa kwa ujumla.
Jiunge na ufuatilie Orijino Komedi kwenye:
Website
www.orijinokomedi.comYouTube
www.youtube.com/orijinokomedi
www.twitter.com/orijinokomedi
Kwamaelezozaidiwasilianana:
Tabasamu Pr Consultancy
0 Comments