WADAU
wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) wameshauriwa kujitokeza
kuchukua fomu za kuwania nafasi mbali mbali za uongozi wa chama hicho
baada ya viongozi waliopo madarakani kumaliza muda wao.
Hadi jana hakuna mgombea aliyejitokeza kuchua fomu za ugombea katika chama hicho ambapo zilianza kutolewa Juni 4 mwaka huu katika Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) jijini Dar es Salaam.
Alisema usaili kwa wagombea ambao watajitokeza kuwania nafasi za uongozi utafanyika Julai 5 kabla ya kuanza kwa taratibu za uchaguzi wa chama hicho ambapo wanachama na wadau mbalimbali watashiriki uchaguzi huo.
Fomu zinazotolewa ni kwa nafasi ya Rais, Makamu, Katibu Mkuu, Mweka Hazina na wajumbe tisa na gharama za fomu hizo kwa nafasi ya Rais sh 150,000, Makamu, Katibu Mkuu, Mweka Hazina ni sh 100,000 na 50,000 kwa wajumbe.
0 Comments