Mama Kanumba na Lulu wakiwa wamekumbatiana baada ya misa maalum ya kumuombea marehemu Kanumba
Wapenzi wa filamu za kitanzania walioko jijini dar es salaam, leo hii
walipata fursa ya kuungana na wasanii mbalimbali wa filamu nchini katika
kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja toka kufariki kwa msanii nguli wa
filamu nchini Steven Kanumba ambaye alifariki tarehe kama ya leo mwaka
mmoja uliopita.
Tukio hilo lilihudhuriwa na watu kibao ambapo pamoja na mambo mengine,
watu mbalimbali walipata fursa ya kuweka mashada ya maua kwenye kaburi
la marehemu, wakiongozwa na mama mzazi wa msanii huyo pamoja na binti
Elizabeth Michael “Lulu”, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kushiriki
katika kifo cha msanii huyo.
Hapa ni baadhi ya picha za tukio hilo kama ambavyo Lenzi ya Michezo
imezipokea toka kwa mdau mkubwa wa filamu nchini Oscar Mpejiwa wa Bongo
Film Data Base
|
NDUGU, Jamaa na marafiki wa aliyekuwa Nguli wa Filamu nchini,
Stive Kanumba, leo wamejumuika kwa pamoja katika kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu staa huyo wa filamu alipofariki
dunia.
Ikiwa ni mwaka mmoja tangu kutokea kwa msiba huo, leo pia
mashabiki wa filamu za kibongo waliohudhuria hafla ya
kumbukumbu hiyo kwa pamoja kuweka mashada ya maua katika
kaburi la Kanumba, wamewashuhudia Mama Kanumba na
Msanii Elizabeth Michael 'Lulu' wakiungana na kuwa kitu kimoja
na kuondoa tofauti zao na kuadhimisha kumbukumbu hiyo kwa
kuwaongoza watu waliohudhuria.
Katika Hafla hiyo walihudhuria pia wasanii kibao wa Filam, ambao
pia walipata fulsa ya kuweka mashada ya maua. |
0 Comments