KUMBUKUMBU NA KISOMO CHA YA HITIMA YA MZEE KARUME MJINI ZANZIBAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,akisalimiana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisdiwandui Mjini Unguja kuhudhuria katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.

Askari wakijipanga kupoea viongozi waliokuwa wakiwasili mahala hapo.
Rais Jakaya Kikwete, akiweka Shada la Maua katika kaburi, wakati wa shughuli hiyo.
Mjukuu akiweka Shada la maua katika kaburi.
Rais Jakaya Kikwete, akiwaongoza makamu wake na Rais wa Zanzibar, na viongozi wengine kuomba dua wakati wa shughuli hiyo.
Sehemu ya Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria kisomo cha Hitima Kumuombea Dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya CCm Kisiwandui Mjini Zanzibar,ambapo kila ikifika siku kama hii wananchi kwa ujumla wao hukusanyika kuomba dua kama hii.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisdiwandui Mjini Unguja kuhudhuria katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.Zaidi Bofya HAPA chini

Post a Comment

0 Comments