Muigizaji
wa filamu nchni, Kajala Masanja, ambaye hivi karibuni alinusurika
kwenda jela baada ya kutolewa faini ya sh. mil.13 na msanii mwenzake,
Wema Sepetu, ameamua kujichora tattoo yenye jina la mfadhili wake huyo
mgongoni, Wema kama ishara ya kumshukuru.
Kajala amejichora tattoo hiyo upande wa kushoto mwa bega lake.
Baadhi
ya wadau wa sanaa wamechangia juu ya kitendo hicho na kusema kuwa,
wanahisi jambo zuri la kulipa fadhila angalau msanii huyo angekuwa na
subira angalau hapo baadaye atakapojaaliwa kupata mtotot mwingine basi
ampe jina hilo, ambapo angekuwa amejiwe mahala pazuri kwa wengi kumhofia
baadaye kupatwa na ugonjwa wa ngozi kwa kujichora Tattoo hiyo.
"Hicho
ni kitu cha muda tu, me naona Kajala angefikiria mbali zaidi kabla ya
kuchukua maamuzi hayo, kwani yanaweza kumsababishia madhara makubwa hapo
baadaye, tunajua analipa fadhila na kuonyesha heshima na shukrani
lakini si kujichora tattoo ambazo si tamaduni zetu waafrika ama
wabongona hasa ukiangalia issue yenyewe iliyokuwa ikimkabili mahakamani
ilikuwa ni serious sana". alisema mmoja wa wadau
0 Comments