NGOWI MSIMAMIZI UBINGWA WA DUNIA



Na Elizabeth John
RAIS wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi anatarajia kuwa msimamizi Mkuu katika pambano la ubingwa wa dunia la vijana katika jiji la Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.

Ngowi anatarajiwa kuwa msimamizi Mkuu katika mpambano huo utakaowakutanisha mabondia Ilunga Makaba kutoka Jamhuri ya Kidokrasia ya Kongo (DRC) mwenye makazi yake nchini Afrika ya Kusini na Gogita Gorgiladze anayetoka katika jiji la Tiblis, nchini Georgia.

Ngowi alisema, pambano la wawili hao wenye wiwango vinavyolingana Georgita (12) na Makaba (12) watapambana kugombea mkanda wa vijana wa wa dunia (Youth Title) wa Shirikisho la Ngumi la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika uzito wa Cruiserweight Februari 15 mwaka huu katika hoteli ya nyota 5 ya Emperors Palace in Kempton Park, Gauteng katika jiji la Johannesburg.

Ngowi kama kamishena mkuu wa pambano hilo atasaidiwa na maofisa wafuatao ambapo mwamuzi ni Wally Snowball, Jaji namba moja Simon Xamlashe na namba tatu Jaap Van Niewenhuizen wote kutoka (Afrika Kusini) pamoja na  Jaji namba mbili Manuel Maritxalar (Spain).

Aliongeza kuwa pambano hilo ni kati ya mapambano zaidi ya 100 ya IBF yatakayofanyika katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika kipindi cha mwaka huu wa 2013 chini ya uradi wa IBF

Post a Comment

0 Comments