JANUARY 28, 2013
Mtanzania
Fadhili Majia sasa atamvaa Mghana Isaac Quaye tarehe 8 March kutafuta nafasi ya
kugombea mkanda wa ubingwa wa Jumuiya ya madola (CBC) ambayo unashikiliwa na
bondia Kevin Satchell wa Uingereza.
Mpambano wa Majia na Quaye umemsogezwa
mbele kwa kuwa mashindano ya ubingwa wa Afrika yanayoendelea nchini Afrika ya
Kusini yanarushwa na televisheni ya Super Sports ambayo ndio wafadhili wakubwa
wa mpambano wao.
Wakati huo huo bondia Richard Commey wa
Ghana atamvaa Mghana mwenzake Bilal Muhammed kugombea mkanda wa IBF katika bara
la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati uzito wa lightweight siku hiyo
hiyo March 30. Aidha bondia Frederick Lawson wa Ghana atazichapa na bondia
Isaac Sowah wa Ghana kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya
Uajemi na Mashariki ya Kati katika uzito
wa Welterweight. Mapambano hayo yatasimamiwa na Rais wa IBF katika bara la
Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi
Mtanzania mwingine atakaye peperusha
bendera ya taifa siku hiyo ni pamoja na Allan Kamote atakayezichapa na bingwa
wa zamani wa IBF wa mabara na ambaye ndiye bingwa wa sasa wa WBA wa mabara
Emmanuel Tagoe katika pambano lisilo la ubingwa.
Naye bondia wa Kenya Michael Odhiambo
atachuana vikali na Mghana George Ashire katika mpambano usio wa ubingwa uzito
wa lightweight.
Mapambano hayo yote yatakuwa ni ya
utangulizi katika mpambano wa ubingwa wa dunia kati ya bondia maarufu wa Ghana
anayeishi nchini Marekani Joseph Agbeko na Luis Mendelez kutoka nchini
Columbia.
IBF/Afrika inawaomba watanzania kwa
ujumla wao wawaombee mabondia wake ili waweze kupeperusha vyema bendera ya
taifa.
Imetolewa na:
UTAWALA
International Boxing Federation Africa
DAR-ES-SALAAM
0 Comments