REDDS Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred ameondoka jijini Dar es Salaam, leo tarehe 12 Desemba 2012 kuelekea mkoani Kagera kwa shughuli za Jamii.
Mrembo
huyo wa Redds Miss Tanzania, akiwa mkoani Kagera atatembelea Shule
maalum ya Mugeza Mseto, inayofundisha wanafunzi wenye ulemavu, pia
atatembelea Kituo cha Nusura ambacho kinatunza watoto yatima.
Mrembo
Brigitte Alfred, ambaye pia ni Balozi wa Walemavu wa ngozi, [Albinos]
atatoa misaada ya kijamii katika vituo hivyo. Vifaa hivyo ni pamoja na
Fimbo maalum za kutembelea walemavu wasioona, Miwani, Kofia na Madawa ya
ngozi kwa ajili ya Walemavu wa ngozi. Pamoja na vyakula.
Redds
Miss Tanzania 2012 pia atatembelea Wilaya ya Misenyi na kutoa misaada
kama hiyo katika kituo kimoja kilichopo wilayani humo.
Ziara ya Miss Tanzania 2012 imedhaminiwa na Optima Lodge & Safaris pamoja na Victoria Perch Hotel zote za Mkoani Kagera.
Kabla ya kurejea jijini DSM Redds Miss Tanzania 2012 ataelekea Mwanza kwa shughuli zingine za kijamii.

0 Comments