DAR ES SALAAMJ, Tanzania
Mamlaka
ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imesema itawakamata
wamiliki wa magari wote watakaohusika katika kupandisha nauli hovyo hvyo.
Msemaji wa Mamlaka hiyo, David
Mziray amesema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati alipokuwa akizungumzia taarifa kuwa kuna baadhi ya madereva na
makondakta kupandisha nauli kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
Alisema
wamejipanga vizuri kwani wamewaandaa vijana watakaoshirikiana na Jeshi la
Polisi ili kuzikamata kampuni za mabasi ambazo zitabainika kupandisha nauli
kinyume cha sheria.
Mziray
alisema katika kipindi hiki wataendesha opresheni kila siku ya kukamata kampuni
ambazo zitaenda kinyume na mkataba wao wa
leseni, itatozwa fani ya sh
25000.
Sambamba
na hilo, aliwatahadhalisha wamiliki wa magari hayo kuwa makini ili kuepuka
kutozwa faini ambazo kwa kiasi kikubwa zinaumiza wao na wala siyo madereva na
makondakta.
“Nafahamu
kweli kuna baadhi ya magari hivi sasa yamekwishaanza kupandisha nauli kutokana
na kuongezeka kwa abiria wanaosafiri kwenda kuungana na familia zao katika
kipindi cha kusherehekea Sikukuu ya X-mas”alisema.
Mziray
alisema SUMATRA haitasita kuzifutia leseni kampuni ambazo zitaonekana kuwa sugu
katika kujiingiza kwenye vitendo hivyo vya kupandisha nauli kwani kwa kufanya
hivyo ni sawa na kuwaibia wananchi.
Vile
vile aliwaasa abiria kutoa ushirikiano
katika operesheni hiyo ya kuzikamata kampuni zinazojihusisha na upandishaji huo
wa nauli, wakati mwingine wanashindwa kutekeleza majukumu yao kutokana na
abiria wenyewe kuwa wagumu kuwafichua madereva na makondakta wanaofanya hivyo.
Hata
hivyo, Mziray alitoa wito kwa wananchi
kupanga nasafari zao kwa utaratibu na wala siyo kurupuka kwani mara nyingi wale
wanao kurupuka kwa kutaka kusafiri siku hiyo hiyo ndiyo maranyingi wanaokumbana
na ubabaishaji huo katika kupata tiketi.
0 Comments