Mkurugenzi wa Benki ya Azania, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (Usimamizi
wa Hazina na Maendeleo ya Biashara) Bw. Godwin Seiya
(kushoto) akikabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa Mratibu wa kampeni dhidi ya Saratani ya tezi dume inayojulikana
kama ‘Tanzania 50 Plus Campaign’ Dk.Emmanuel Kandusi (katikati)
ikiwa ni msaada wa benki hiyo katika Kampeni hiyo. Kulia ni Mratibu kutoka
Shirika lisilo la kiserikali la SAHRiGON Martina Kabisama.
Na Mpiga Picha Wetu.
Na Mpiga Picha Wetu.
Mkurugenzi wa Benki ya Azania, Ofisi ya Mkurugenzi
Mtendaji (Usimamizi wa Hazina na
Maendeleo ya Biashara) Bw. Godwin Seiya (katikati)
akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa Mratibu wa kampeni dhidi ya Saratani ya tezi dume inayojulikana
kama ‘Tanzania 50 Plus Campaign’ . Kushoto ni Mratibu wa kampeni hiyo Dk.Emmanuel Kandusi na kulia ni Mratibu kutoka Shirika lisilo la kiserikali la SAHRiNGON
Martina Kabisama.
Mratibu wa kampeni dhidi ya Saratani ya tezi dume
inayojulikana kama ‘ Tanzania 50 Plus Campaign’ Dk.Emmanuel Kandusi (kushoto) akisisitiza jambo kwa
wanaandishi wa habari kabla ya kupokea hundi ya shilingi milioni tano kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya Azania
katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (Usimamizi wa Hazina
na Maendeleo ya Biashara) Bw. Godwin Seiya (katikati) ikiwa ni msaada wa
benki yake katika Kampeni hiyo.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya
Azania imechangia shilingi milioni tano kuiunga mkono kampeni ya
Tanzania 50 Plus inayolenga kujenga uelewa kwa wananchi dhidi ugonjwa wa
saratani ya tezi dume (Prostate Cancer).
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Benki ya Azania, ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (Usimamizi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara) Bw. Godwin Seiya alisema benki yake itaaendelea kusaidia programu mbalimbali za kijamii ndani ya jamii inayoizunguka benki hiyo.
Alisema benki
yake ipo katika mchakato wa kuandaa sera maalum itakayo simamia shughuli
mbalimbali za benki zinazolenga kuisaidia jamii na kusisitizia kuwa
sera hiyo itaeleza kikamilifu mchango wa benki yake kwenye suala la
kusaidia miradi mbalimbali ya kijamii huku akisema kuwa uamuzi huo
utafikiwa baada ya makubaliano na wanahisa wa benki hiyo.
Alibainisha
kuwa benki yake imeamua kusaidia kampeni hiyo ya Saratani ya tezi dume
iliikusaidia kuhamasisha wananchi kufanya vipimo angalau mara moja kwa
mwaka, na kuongeza kuwa kupitia jitihada hizo itsaidia kupunguza hatari
ya kuwa na waathirika wengi wa ugonjwa huo sbaadae.
"Takwimu
zinasema ni watu 1000 wanaofariki kwa ugonjwa wa saratani kila mwaka
Tanzania.Saratani ya tezi dume imaua mwanaume moka kila dakika 13. Sisi
kama Benki ya Azania tunaamini kuwa njia pekee ya kupunguza hathari ya
ugonjwa huu ni kupitia kampeni ya kujenga uelewa katika jamii.
"Kwa minajili
hiyo basi sisi kama Benki ya Azania tunaona namna moja ya kudhibiti ni
kwa uenezi wa taarifa zake kwa watu wachukue tahadhari paaale
inapowezekana kuepukana na ugonjwa huu," aliongeza.
Kwa upande
wake Mratibu wa kampeni hiyo ya Tanzania 50 Plus Dk.Emmanuel Kandusi
ambae pia ni muhanga wa saratani ya tezi dume wakati wa tukio hilo
alisema maisha ya watu wengi yataokolewa kama watu wataamua kufanya
uchunguzi wa hiari katika umri mdogo kati ya miaka 45 na 50.
"Ugonjwa huu
ni hatari. Mara nyingi watu wengi huamua kwenda hospitali pale ugonjwa
unapofikia hatua mbaya. Ni muhimu kwa wnaume wenye umri wa takribani
miaka 50 na kuendelea kuweka kipaumbele tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa
saratani ya tezi dume angalau mara moja kwa mwak, "aliongeza.
Aidha, Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la SAHRiNGON Martina Kabisama alitoa wito kwa makampuni mengine na watu binafsi kuiunga mkono kampeni hiyo ili kampeni hiyo ilete matokeo yaliyo chanya kwa
0 Comments