BASATA:WASANII JIPANGENI KWA URASIMISHAJI WA SEKTA YA SANAA


Mkuu wa Idara ya Mfuko na Uwezeshajikutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Angelo Luhala (Katikati) akisisitizajambo wakati akieleza umuhimu wa Wasanii kujisajili ili kuwa tayari kwa ajiliya urasimishaji wa Sekta ya Sanaa. Kulia ni Afisa Habari wa BASATA AristidesKwizela na Kaimu Mkuu wa kitengo cha matukio BASATA, Malimi Mashili.

NaMwandishi Wetu
Baraza la Sanaa laTaifa (BASATA) limewataka wasanii kujipanga kwa ajili ya zoezi la urasimishajiwa sekta ya Sanaa linalotarajiwa kuanza ifikapo Januari mwaka 2013.

Wito huo umetolewawiki hii na Mkurugenzi wa Idara ya Mfuko na Uwezeshaji, BASATA Bw. AngeloLuhala wakati akitoa elimu kwa wadau wa Jukwaa la Sanaa kuhusu ‘Urasimishajiwa Sekta ya Sanaa na Hakimiliki’ kwenye Ukumbi wa Baraza hilo uliokoIlala Sharif Shamba

Alisema kuwa, wasaniihawana budi kujipanga kuondoka kwenye mazingira ya kufanya kazi kiridhaa napasipokuwa rasmi bali wanyanyuke na waseme sasa Sanaa ni kazi inayopaswa kupewaheshima yake kama kazi zingine.
“Wasanii tuondokekwenye ridhaa, tuseme Sanaa ni kazi kama zilivyo kazi zingine, tuunge mkonojitihada za Serikali za urasimishaji sekta ya Sanaa ifikapo mwezi Januarimwakani ili kuipa hadhi sekta hii” alisisitiza Luhala.
Alizitaja faida zaurasimishaji sekta ya Sanaa kuwa ni pamoja na kazi zote za Sanaa kutambuliwakupitia kuwekewa stika maalum na mamlaka ya mapato nchini (TRA) ili kudhibitiuharamia lakini pia kusaidia kupata takwimu sahihi za sekta na kuchangia patola taifa

“Kuanzia Januarimwakani sekta hii itaanza kurasimishwa. Hii ina maana kuwa, kazi za wasaniizitawekewa stika na TRA ili kudhibiti uharamia. Aidha, mapato yatokanayo naSekta ya Sanaa yatakuwa bayana kwa Serikali ili kurahisisha upatikanaji watakwimu na kupanga mipango ya maendeleo ya Wasanii” aliongeza Luhala.
Alizidi kueleza kuwa,zoezi la urasimishaji sekta ya Sanaa ambalo limekuwa likipigiwa chapuo nawasanii wenyewe halitakuwa na maana kama wasanii hawatajitokeza kwa nguvu zotena kuunga mkono juhudi za Serikali.
Mbali na Wasanii,Luhala alizitaja kumbi za Sanaa na burudani, makampuni ya ukuzaji sanaa(mapromota), vikundi vya Sanaa, studio za kurekodia muziki na filamu, wachorajiramani za majengo na wapigapicha kama wadau wengine wanaotakiwa kurasimishwakupitia kusajiliwa na kupewa vibali.

Kwa upande wa wadauwaliochangia mjadala huo walipongeza hatua hiyo ya Serikali kuona umuhimu wakurasimisha sekta ya Sanaa lakini wakahoji zoezi hilo kugusa Sanaa za filamu namuziki pekee.

“TunaipongezaSerikali kwa kujipanga kurasimisha Sekta ya Sanaa lakini ni vema Sanaa zaUfundi na Maonesho nazo zikahusishwa kwenye mchakato huu badala ya filamu namuziki pekee” alishauri NKwama Balanga.

Post a Comment

0 Comments