Sisi Wanachama wa YANGA kupitia TAWI LA UHURU tunapenda kuujulisha umma wa WANA YANGA ya kuwa,
(i) Kwa mujibu ya Katiba yetu iliyopitishwa na Wanachama wa YANGA tarehe 17/06/2010 na kuidhinishwa na msajili wa Vyama Vya Michezo tarehe 15/07/2010.Hakuna kipengele chochote ndani ya Katiba yetu kinachotambua uwepo wa Baraza au Kamati ya Wazee na Vijana ndani ya Club ya YANGA kwa mujibu wa Katiba. Ila kama Wanachama wa YANGA tunatambua uwepo wa Wazee, Vijana na kina Mama ndani ya YANGA na tunaeshimu na kuthamini michango yao ndani ya YANGA
(ii) Kwa mujibu wa Katiba ya YANGA, Ibala ya 33, Kipengele cha 3.a) Mwenyekiti ndiye Kiongozi wmkuu na pia msemaji mkuu wa Club.
(b) Pia ndiye mwenye Mamlaka ya kuitisha mkutano mkuu na mkutano wa Kamati ya Utendaji.
Je! ni wapi Katiba yetu imeelekeza kuwa Kikundi au Mwanachama ana mamlaka ya kuitisha mkutano? Kwa mujibu wa Katiba hakuna.
Ndugu Wanahabari na Wanachama wa YANGA
Ibala ya 22 ya Katiba yetu ya YANGA ndio kimbilio la Wanachama kwa kumtaka Mwenyekiti kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji kutuitishia mkutano mkuu wa dharula kama ibala hiyo ya 22 kipengele cha (ii) kinavyosema na nanukuu:- “Endapo angalau ½ ya wajumbe (Wanachama) wamewasilisha ombi kwa Kamati ya Utendaji na kwa maandishi, Kamati ya Utendaji itawajibika kuitisha mkutano mkuu wa dharura katika kipindi kisichozidi siku 30 baada ya kuwasilishwa kwa ombi hilo” Mwisho wa kunukuu, na Kipengele cha (iii) Kinasema Wito wa mkutano hauna budi kupelekwa angalau siku 15 kabla ya mkutano na kipengele cha (iv) cha ibala hiyo hiyo ya 22 kinaelekeza Ajenda na nyaraka nyingine muhimu zitapelekwa kwa wajumbe angalau siku 7 kabla ya mkutano”.Ndugu Wanahabari na Umma wote kwa ujumla
Kilichofanywa na baadhi ya Wanachama wenzetu siku ya terehe 20/05/2012 ni UHUNI na Upotoshaji mkubwa wa Katiba yetu. Hapa ndipo wana YANGA wanatakiwa kuwa macho na baadhi ya Wanachama wenzetu kwani wanania ya kuturudisha tulipotoka. YANGA ni taasisi kubwa yenye Wanachama wengi makini kwani kwa sasa tuna Wanachama zaidi ya Elfu kumi na mbili (12,000) ambao hatuwezi kuamliwa au kuyumbishwa na Wanachama wachache.Ndugu Wanahabari na Wanachama wa YANGA
Sisi Wanachama wa YANGA TAWI LA UHURU tunawakanya wale wote ambao kwa maslahi Sisi Wanachama wa YANGA TAWI LA UHURU tunaamini matatizo au migogoro ya YANGA itamalizwa kwa kufuata Katiba yetu na kwenye vikao halali na ukiona mtu ataki vikao halali ujue ana matatizo au maslai yake binafsi na si ya YANGA.
Ahsanteni,
DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO
SULTAN BAKARI
KATIBU WA TAWI LA UHURU
23/05/2012.
23/05/2012.
0 Comments