Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, amekutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Terezya Huvisa, kwa mazungumzo na kupokea taarifa ya zoezi la Bomoa bomoa nyumba zilizojengwa maeneo ua Ufukweni, ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni. Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu Dar es Salaam jana Mei 17, 2012. Katika picha kutoka (kushoto) ni Katibu wa Wizara ya Ardhi, Veldiana Mashingia, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka (kulia) ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dkt. Julius Ningu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa, baada ya mazungumzo hayo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
WAZIRI MKUU AKAGUA MADHARA YA MOTO SOKO LA SIMU 2000, AAGIZA HATUA ZA
HARAKA KUREJESHA BIASHARA
-
-Asema Serikali itatoa kauli baada ya uchunguzi
-Aagiza vibanda vipya vigawiwe kwa wafanyabiashara halisi
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza hat...
8 hours ago

0 Comments