Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts inayochapisha gazeti la Jambo Leo, Juma Pinto (katikati) akimpongeza Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (kulia), ofisi za gazeti hili Dar es Salaam jana kwa kupewa tuzo na cheti cha ushiriki viliyotolewa na Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc baada ya kuwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Anayeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Jambo Concepts, Benny Kisaka
. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (kushoto) akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Jamhuri ya Uturuki (Idara ya Habari na Maelezo), Murat Karakaya iliyotolewa kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan, baada ya kuwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
0 Comments