MWANAMUZIKI nyota nchini ambaye anapiga mzigo katika bendi ya Extra Bongo, Rogart Hegga 'Katapila' pichani juu ameelezea kufurahishwa kwake na uwezo wa kisanii wa mwimbaji wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' Ramadhani Athumani maarufu kama Dogo Rama ambapo kwa sasa anatamba na albamu yake aliyoipiga katika mtindo wa ZingZong iitwayo ‘Dogo ‘Rama – Kilometa 10,000’.
Katapila ambaye ni mmoja wa wanamuziki walioshirikishwa katika albamu hiyo, amemsifu Dogo Rama kwa kuwa mjanja na mbunifu ambapo ameweza kuwakutanisha marapa nyota Msafiri Diouf na Yanick Noah 'Sauti ya Radi' ambao wamechuana vikali katika moja ya nyimbo za albamu hiyo na kuupamba wimbo.
"Huyu dogo kweli anaweza kufika mbali kwani anajaribu kufanya kila awezalo katika kuhakikisha ndoto za mafanikio yake zinatimia, ule ushiriki wa vipaji tofauti unasaida kuleta mabadiliko kwa wimbo na kutomchosha msikilizaji wa albamu na kadhalika," alisema Hegga akimmwagia sifa Dogo Rama.
Akaongeza kuwa: "Kama mtu atapata nakala ya albamu hii iliyoingia madukani wiki iliyopita, bila shaka atagundua kuwa huyu dogo ametumia akili yenye mwelekeo wa ukomavu kwa kutokuwa na choyo katika fani. Vilevile, amedhihirisha kuwa na kiu ya maendeleo."
Albamu ya ‘Kilometa 10,000’ imeingia sokoni wiki iliyopita na tayari imekuwa gumzo karibu kila kona ya jiji la Dar es Salaam na mikoani hususan Mwanza ambako Dogo Rama anatoka.Katika albamu hiyo yenye video (DVD) na (VCD), audio (CD) na (Tape) kuna jumla ya nyimbo 6 ambazo ni 'KM 10,000' aliowashirikisha Msafiri Diouf na Sauti ya Radi, 'Siri ya Mapenzi' aliowashirkisha Rogart Hegga na Cantona,'Chuki za Nini?','Baba na Mama' aliomshirikisha Khadija Kimobiteli, 'Imani ya Mapenzi' aliomshirikisha Benno Villa na 'Uzuri Wangu'

0 Comments