Social Icons

Tuesday, March 6, 2012

TUZO ZA DIAGEO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA BIASHARA AFRIKA 2012-(Diageo Africa Business Reporting Awards 2012) ZAZINDULIWA RASMI.

Usajili wa tuzo sasa uko wazi kufanyika kwenye tovuti.

Dar es Salaam - Machi 6, 2012, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), ambayo ni kampuni tanzu ya Diageo, inayoongoza duniani katika biashara ya vinywaji vyenye kileo, leo wamezindua rasmi tuzo za habari za kibiashara kwa mwaka huu 2012.

Tuzo hizi zilianzishwa na Diageo mwaka 2004, kwa ajili ya kuwatambua waandishi wa habari na wahariri ambao wameweza kutoa taarifa zilizojitosheleza na za hali ya juu katika mazingira ya biashara Afrika. Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Bi. Teddy Mapunda alisema “ Kampuni ya Diageo inaamini kwamba taarifa nzuri na sahihi zina mchango mkubwa wa kuinua mtazamo wa maendeleo na uchumi wa Afrika na changamoto zake.” Habari hizo kwa kiasi kikubwa zinahamasisha nia ya kufanya biashara na zinaangaza mazingira mazuri na ya uhakika juu ya utajiri wa bara hili,”alisema Bi Mapunda.

Bw. Nick Blazquez, Rais wa Diageo Afrika, naye alitoa vielelezo kuhusu tuzo hizi na alikuwa na haya ya kusema: “Ni dhahiri kabisa sasa kwamba hamasa ya biashara Afrika imepanuka na dunia nzima sasa imeridhika na kiwango cha ukukuaji wa uchumi baran Afrika. Kama kampuni inayoendesha shughuli za kibiashara Afrika, tunaelewa umuhimu wa kuongezeka kwa taaluma ya uandishi wa habari za kiabishara na jinsi inavyounda mazingira mazuri na kuvutia kwa uwekezaji wa muda mrefu,” aliongeza.

“Nikiangalia miaka ya nyuma na maendeleo ya tuzo hizi, nimetambua uamsho wa hali ya juu na viwango vilivyomo katika uandishi wa habari za kibiashara na kuongezeka kwa juhudi za vyombo vya habari ndani na nje ya Afrika ili kuhamasisha biashara na ujasiriamali barani humu. Ninajivunia kwamba Diageo inatambua mafanikio haya na tunategemea kuona mchango wa hali ya juu kwa siku za usoni.”

Wakati tuzo hizi za waandishi wa habari za biashara Afrika kutoka Diageo zinakaribia kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake, Diageo inaendelea kufikiria jinsi watakavyobadilisha uhalisia, matokeo na namna ya kuwafikia zaidi walengwa wa tuzo hizi.
Diageo inategemea kuboresha zaidi utoaji wa tuzo hizi kupitia mafanikio ya mwaka uliopita, kukaribisha usajili kutoka vyombo vyote vya habari na kutoka bara zima la Afrika na nje ya Afrika.
Mwaka huu, kundi la mfumo mpya wa utoaji wa habari limeondolewa na kuwa kundi linalojitegemea ili kuonyesha upana wa vyombo vinavyotumia mfumo huu wa utoaji habari. Waandishi wa habari wanahamasishwa kutuma maombi yao. Habari ziwe zimetolewa kupitia mfumo wa vyombo vyote vya habari, ikiwa ni pamoja na gazeti mtandazo (blogs) na habari zilizochapishwa kupitia tovuti mbali mbali pia wanaruhusiwa katika makundi yote, yaani 'categories'. Sherehe ya Tuzo hizi zitafanyika mjini London, Uingereza tarehe 28 mwezi Juni. Tarehe ya mwisho wa kupokelewa kwa maombi haya ni siku ya Ijumaa tarehe 23 mwezi Machi mwaka huu. Maombi yote yatumwe kupitia tovuti yetu: www.diageoafricabusinessreportingawards.com. Hakuna kiingilio.

Kutoka kulia ni Meneja  wa Jamii na Mahusiano ya Jamii na Mawasiliano Nandi Mwiyombela, katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano SBL,Teddy Mapunda na  Meneja wa Mawasiliano ya Ndani SBL Imani Lwinga, wakizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani leo Dar es Salaam.

No comments:

 
 
Blogger Templates