Natoa shukrani zangu za dhati na kwa niaba ya familia ya ndugu Said Tamimu Ally. Nashukuru sana kwa wote waliotoa michango yao ya mali na hali kwa ajili ya kumsaidia ndugu yetu Tamimu.Shukrani pekee ziwaendee ndugu walioko UK,Norway, Muscat, Dar es salaam,Tabora,arusha na sehemu nyinge nyingi kwa msaada wao wa hali na mali ikiwemo ushauri na kutoa pole.
Pili ningependa kuwajulisha kuwa kaka Tamimu siyo mtoto nadhani nilipotuma kwenye glob nilisahau kutaja umri.Huyo ni mtu mzima mwenye mtoto mmoja wa darasa la saba.Mimi siyo mzazi ila nilimfahamu wakati anapata matibabu hospitali ya KCMC Moshi. .Baada ya kumuona anatatizo niliendelea kunfuatilia mpaka alipo pata referal kwenda Ocean Road Hospital. Kwa sasa hali yake inaendelea kuzorota kwani ameniambia alikwisha maliza kupata mionzi 20 ambayo ameandikiwa pale Ocean Road Hospital, anakwenda na kurudi siku ya clinic.
Nashukuru kwa mawazo ya wengi nimeweza kufungua account benki ya NMB Magomeni ambayo msimamizi ni mdogo wake aitwae Fatuma Tamimu. Ametoa idhini account ifunguliwe kwa jina la mdogo wake wa kike kwani mtoto wake ana umri wa chini ya miaka 18. Kwa wale wote waliotumia M-Pesa,Tigo pesa na Western Union nimekabidhi pesa kwa ndugu Tamimu. Kwa niaba yake natoa shukrani za dhati ,asanteni sana .Lakini kwa vile tumefungua accout basi watakaoguswa watumie account number hii
20510000732
NMB Magomeni Branch
Fatuma Tamimu
Mwenyezi Mungu awazidishie wote
Anna Sangai
picha zaidi kuona BOFYA HAPA
Ahmad Issa Michuzi
P.O BOX 4156,
DAR ES SALAAM.
http://www.michuzijr.blogspot.com/
Phone:0713 422 313/ 0783 422 313
Tanzania- East Africa.
0 Comments