UWANJA WA KAUNDA KUBEBA MASHABIKI 15,000

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Lyoid Nchunga akibadilishana hati na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NEDCO Construction Ambwene Mwakyusa kulia ni Katibu Mtendaji wa Yanga Celestine Mwesigwa

UONGOZI wa mabingwa Soka Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam umesaini mkataba wa awali na kampuni ya NEDCO Construction kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wake kisasa wa Kaunda utakaokuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 15,000 wakiwa wamekaa sambamba na jengo la kibiashara la ghorofa saba.
Utiliaji saini wa mkataba huo umefanyika jijini Dar es Salaam jana, ambako kampuni hiyo imepewa jukumu la kuandaa michoro ya ujenzi wa uwanja huo na jengo la kibiashara la Mtaa wa Mafia ikiwamo kutoa tathimini ya gharama za jumla zitakazotumika kukamilisha mradi huo.

Post a Comment

0 Comments