UNDER 20 'NGORONGORO HEROES' KWENDA GABORONE BOTSWANA LEO JIONI

Kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya Taifa  ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes na viongozi watano kinatarajia kuondoka kesho (novemba 30 mwaka huu) kwa ndege ya PrecisionAir kwenda Gaborone, Botswana.


Ngorongoro Heroes itaondoka saa 20.20  leo usiku kupitia Johannesburg, Afrika Kusini kwenda huko kushiriki michuano ya umri huo ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA).

Michuano hiyo itafanyika kuanzia Desemba 1-10 mwaka huu ikishirikisha timu za mataifa 11 wanachama wa COSAFA na Tanzania inayoshiriki kama mwalikwa.

Wachezaji watakaoondoka ni Saleh Malande (Simba), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Suagr), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Said Samir (Kagera Sugar), Samuel Mkomola (Azam), Frank Domayo (JKT Ruvu Stars) na Omega Seme (Yanga).

Wengine ni Atupele Green (Yanga), Jerome Reuben (Moro United), Simon Happygod (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Abdallah Hussein (AFC), Rajab Mohamed (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba), Emily Josiah (TSC Mwanza), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting Stars).

Ngorongoro Heroes iko kundi C pamoja na Zambia, Afrika Kusini na Mauritius na itacheza mechi yake ya kwanza Desemba 2 mwaka huu dhidi ya Zambia. Mechi ya pili itakuwa Desemba 4 mwaka huu dhidi ya Afrika Kusini wakati ya mwisho katika hatua hiyo ya makundi ni dhidi ya Mauritius itakayochezwa Desemba 6 mwaka huu.

Msafara wa timu hiyo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Muhsin Balhabou. Wengine katika msafara huo ni Kocha Mkuu Kim Poulsen, Kocha Msaidizi Mohamed Rishard, Daktari wa timu Dk. Joakim Mshanga na kocha wa makipa Peter Manyika.

Post a Comment

1 Comments

JigambeAds said…
Tunawatikia vijana wa Ngorongoro Hereos U20 wafike salama katika safari yao, na waweze kucheza mpira mzuri na kutoka na ushindi mzuri!