Sisi kama wanafunzi ambao tunaathirika na mgomo huu Bado tuna imani na Serikali ya Mh.Jakaya kikwete na watendaji wake wote, Katibu Mkuu Wizara ya elimu,Tanzania Commision of Universties na Higher Education Student Loan Board tunawaomba waumalize mzozo huu.
Pesa nyingi zimetumika za walipa kodi kupitia loan board kuwakopesha wanafunzi hawa Tunahitaji sasa wote kwa pamoja kulishughulikia hili tatizo ili tuweze kuendelea na Masomo na mwisho tuende kujenga taifa letu changa lenye upungufu mkubwa wa Madaktari.
Ni jambo la kusikitisha sana kuona nchi ambayo ina upungufu mkubwa wa Madaktari, kushindwa kuumaliza mgomo wa Madaktari Wanafunzi ambao sasa umekamilisha miezi miwili, kundi hili la wanachuo limekuwa likikusanyika nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Elimu kwa vipindi tofauti bila hitimisho la mgomo huu.
Kwa kutambua umuhimu wa wataalam hawa tunaziomba mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia na kuongoza ziumalize mzozo huu ambao madai yao ya msingi ni kulipa Ada kwa Tshs na si US Dollar na pia kulipa ada kubwa tofauti na vyuo vingine vya binafsi (private).
0 Comments