Mwenyekiti wa Tanzania Gives Back,Edmond Lyatuu akizungumza na baadhi ya wazee wenye ulemavu wa mikono,macho na miguu kutokana na kuathiriwa na ugonjwa wa Ukoma,Wazee hao wametoa kilio chao kwa Serikali na wadau mbalimbali kwamba wajitokeze kuwasaidia wazee wao kwa namna moja ama nyingine,kwani kwa sasa wamekuwa wakiishi katika hali ngumu hivyo bado wanahitaji msaada mkubwa wa hali na mali.
Mwenyekiti wa kampeni ya Tanzania Gives Back 2011,Edmond Lyatuu pichani kulia akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya usafi mapema leo asubuhi kwa baadhi ya wazee waishio kwenye kambi ya Walemavu na Wasiojiweza ya Nunge,Vijibweni-Kigamboni jijini Dar es salaam.
Pichani na ni baadhi ya wazee wakiwasikiliza wageni wao waliofika kuwatembelea mapema leo asubuhi.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ditto akiimba moja ya wimbo wa kuwafariji na kutia moyo wazee hao ambao wengi wao wameathiriwa na ugonjwa wa ukoma.Wazee hao wanaishi kwenye kijiji hicho cha Nunge chenye jumla ya nyumba 50,ikiwa na idadi ya familia 72,ambapo kila nyumba inakaliwa na watu 5 mpaka 7.Akizungumza kwa niaba ya wenzake Mzee Issa Ally ameiomba Serikali na wadau wengine kuja kuzikabarabati nyumba zao wanazoishi kwani kwa sasa zimechakaa sana,amesema na kuongeza kuwa wanahitaji msaada mkubwa wa kupuliziwa dawa ya kuuwa wadudu katika nyumba zao,kwani kumekuwepo na wadudu wengi wakiwemo Viroboto,Mende na wengineo ambao wamekuwa wakiwapa taabu sana.
Kulia ni mwendeshaji wa kipindi cha Njia Panda kinachorushwa na redio ya Clouds FM,Dr Isaac Maro akiutazama mguu wa Mzee Rasmo Kilata ambaye mguu wake ulikatwa mara baada ya kuathiriwa na ugonjwa kansa,ambao ulitokana na kidonda chake alichokipata kwa muda mrefu bila kupona,Mzee huyo wa makamo mwenye watoto 3 na wajukuu wasio na idadi pia ni mlemavu wa ugonjwa ukoma,Shoto ni Mwenyekiti wa Kampeni ya Tanzania Gives Back,Edmond Lyatuu akiwa pamoja na mratibu wa Kampeni hiyo,Dada Susan,kampeni hiyo ya Tanzania Gives Back 2011 inaratibiwa na kituo cha Tanzania House Of Talent (THT).
0 Comments