Social Icons

Wednesday, September 28, 2011

KUNDI LA MUTATI KUTOKA KENYA LAWASILI MAHSUSI KWA KUNOGESHA SHEAR CHARITY BALL 2011

 Wasanii wa kundi la mutati  wakilakiwa na mwenyeji wao kutoka Kampuni ya Shear Illusions Dora Raymond .
 Wasanii wa miondoko ya Salsa wa kundi la Mutati la nchini Kenya wakiwasili  leo jioni katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, wasanii hao wataburudisha katika hafla ya Shear Ball itakayofanyika  Jumamosi  katika Hoteli ya Movenpick.
Hafla hiyo inalenga kuchangisha milioni 50 za kusaidia ukarabati wa mfumo wa maji taka katika hospitali ya Mwananyamala pamoja na kusaidia fedha za matibabu kwa wanawake wenye kuugua ugonjwa wa fistula.

 Wasanii hao wanne ni Yassin Mutati aliyevaa njano, Triza Wanjeri, Alice Kang'ara na Daniel Mutema.
 Wakielekea vyumbani kupumzika mara baada ya kuwasili katika hoteli ya Peacock ambayo ni mmoja kati ya wadhamini.
Wasanii wa kundi la Mutati wakiwa katika picha ya pamoja na Head of Marketing and Corporate Affairs Dorah Raymond (wa pili kushoto).

No comments:

 
 
Blogger Templates