KLABU za ngumi za ridhaa za Ashanti na Amana zimewataka vijana wenye vipaji vya mchezo huo kujitokeza kujiunga na klabu hizo ili kuendelezwa vipaji vyao.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha mkuu wa Klabu ya Ashanti Rajab Mhamila 'Super D' alisema kutokana na kugundua kuwepo na vijana wenye uwezo mkubwa wa kucheza ngumi na kukosa watu wa kuwaendeleza hivyo wameona ni fursa pekee ya kuwachukua na kuwaendeleza katika Klabu zao.
Alisema, baada ya mkoa wa kimichezo wa Ilala kuanzisha mapambano ya kuhamasisha mchezo huo wameona vijana wengi waliokuwa na moyo wa kutaka kucheza mchezo huo hivyo wameona watoe nafasi kwa vijana hao kujiunga katika Klabu zao.
"Mimi na kocha wa Klabu ya Amana, Habibu Kinyogoli tumeamua kwa nia moja kuiwaendeleza vijana katika ngumi hizi hivyo tumeona tutoe nafasi kwa vijana wenye kipaji cha ngumi kujitokeza kujiunga na klabu zetu bila gharama zozote ikiwa ni kwa lengo la kuendeleza vipaji vyao," alisema Super D.
Alisema, mabondi hao watapata nafasi ya kupambana ulingoni mbele ya mashabiki huku katika mafunzo wakiwa wananolewa na yeye akiwa pamoja na Kinyogoli na Kondo Nassoro ambapo wote ni makocha wa kambi ya mkoa wa Ilala.
Aliongeza kuwa wakiwa ni waanzilishi wa ligi ya kuhamasisha ngumi hizo kwa mkoa wa Ilala na Dar es Salaam kwa ujumla wameamua kuendelea kupanua wigo huo kwa kuongeza idadi ya mabondia pia katika klabu zao.
(SUPER D)
DIRECTOR
http://www.burudan.blogspot.com/
BURUDANI MWANZO MWISHOP.O Box 15493
DAR ES SALAAMPhone no. 0713/0754/0787/0774/ 406938
Timu ya Yanga Yatinga Fainali Michuano ya NMB Mapinduzi Cup 2026 Kwa
Kuifunga Timu ya Azam Bao 1-0, Mchezom Uliyofanyika Uwanja wa New Amaan
Complex Zanzibar
-
Mchezaji wa Timu ya Azam akimiliki mpira huku beki wa Timu ya Yanga
akijaribu kumzuiya wakati wa mchezo wa nusu fainali ya michuano ya NMB
Mapinduzi Cup ...
7 hours ago
0 Comments