Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi kipya kutoka jijini Dar es Salaam , Juma Nature juzi alikonga nyoyo za washabiki wa muziki huo vilivyo katika tamasha maalum lililoandakiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Nane Nane mjini Mbeya.
Katika tamasha
Kadri alivyokuwa akizidi kutoa burudani ndivyo washabiki walivyokuwa wakipandwa na mzuka hadi kufikia hatua ya kukata uzio uliokuwa mbele ya jukwaa huku kila mtu akitaka kumshika mkono. Hali hiyo ilisababisha Nature kusimamisha burudani kwa dakika kadhaa ili kurudisha hali ya utulivu na hatimaye burudani ilirejea katika hali yake ya kawaida.
Mbali na Nature na kundi lake la TMK Wanaume family, mwanamuziki mwingine aliyeonyesha uwezo mkubwa jukwaani katika stahili ya muziki wa kizazi kipya kutokana na kushangiliwa na umati kila mara ni Roma Mkatoliki kutoka Tanga ambaye alipanda jukwaani baada ya Nature na kundi la TMK Wanaume family kumaliza kutoa burudani.
Akiongea baada ya Tamasha hilo Meneja wa Mauzo wa Tigo wa mikoa wa Mbeya na Rukwa Kevin Mibazi alisema kuwa mbali na kuadhimisha sikukuu za Nane Nane, tamasha hilo pia lilikuwa la kuwashukuru wateja wa Tigo kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani.
”Ndiyo maana katika tamasha ili tumeamua kutoa huduma zetu kwa bei ya chini ili kila mtu apate huduma zetu kwa bei inayo kubalika, kwahiyo tunatumia fursa hii kuleta burudani ya wasanii wakubwa, na kama ulivyoona wanapendwa
Katika tamasha
Kwa mujibu wa Mibazi matamasha kama hayo yameishafanyika katika baadhi ya mikoa na yanatarajiwa kuendelea katika mikoa mingine hapa nchini kama sehemu ya kuhamasisha huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni ya Tigo.
Sehemu ya umatiKR wa Wanamue TMK jukwaani
Roma akipagawisha jukwaani
Meneja wa mauzo mikoa ya Mbeya na Rukwa Kevin Mibazi (kulia) akimkabidhi zawadi ya simu ya mkononi mmoja wa washindi wa kusakata kiduku Monica Jonas.
0 Comments