MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Z. Anton anatarajiwa kuwaburudisha mashabiki wake wa mji wa Kibaha mkoani Pwani katika shamrashamra za sikukuu ya Idd el Fitr.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, Z. Anton alisema kuwa, onyesho hilo litafanyika kwenye ukumbi wa Masai Park siku ya Idd mosi.Alisema kwamba onyesho hilo limeandaliwa na Kampuni ya Daz
Entertainment na kwamba yeye kwa upande wake, amejiandaa kutoa burudani ya hali ya juu kwa wote watakaojitokeza kuhudhuriaOnyesho hilo.Alisema kuwa kiingilio katika onyesho hilo kitakuwa sh. 4,000, kwa kila mtu na akawaomba mashabiki na wapenzi wote wa burudani wa mji wa Kibaha na vitongoji vyake kujitokeza kwawingi siku hiyo.
KENYA YATOA HATI ZA VYUO VIKUU KWA KAIST NA KEMRI
-
*Na Mwandishi Wetu*
*Serikali ya Kenya imetoa hati rasmi za vyuo vikuu kwa Kenya Advanced
Institute of Science and Technology na Kenya Medical Research I...
7 hours ago

0 Comments