MAPACHA WATATU KULA EID PILI MAILIMOJA KIBAHA

BENDI ya muziki wa dani ya Mapacha Watatu wanatarajiwa kutoa burudani  ya aina yake siku ya Idd pili kwenye ukumbi wa Contena Maili Moja Kibaha Mkoani Pwani.
Aidha ifikapo  Septemba 2 katika ukumbi wa HillTech Ukonga Banana.Kwa mujibu wa Mratibu wa onyesho hilo Sauda Mwilima alisema kuwa bendi hiyo itatambulisha nyimbo zake tatu ambazo ni ‘Usia wa Babu’, ‘Wivu’, ‘Sumu ya Mapenzi Remix na Mtoto ‘Mtoto wa Paka’.Sauda aliongeza kwa kusema kuwa katika onyesho hilo watatambulisha waimbaji wake wapya waliojiunga na bendi hiyo ambao ni Januari na Kambi.Bendi ya Mapacha watatu imeasisiwa na wasanii watatu ambao ni Kalala Hamza Kalala ‘Kalala Junior’ , Khalid Chuma ‘Chokoraa’ na Jose Mara.

Post a Comment

0 Comments