BENDI YA EXTRA BONGO KULA EID MEEDA CLUB SINZA MORI

Bendi ya muziki wa Dansi Extra Bongo Next Level Wazeee wa Kizigo inatarajia kula sikukuu ya EID EL FITRI katika Ukumbi wa Meeda Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki juu pichani alisema, kiingilio katika onyesho hilo kitakuwa sh. 5000 ambapo aliwataka mashabiki na wadau wa muzioki huo kujitokeza kwa wingi ili kuburudika na nyimbo zao mpya ambazo ni 'Mtenda Akitendewa', 'Ufisadi wa Mapenzi' na 'Watu na Falsafa' bila kusahau zile za zamani '3x3', 'Double Double', 'Fikiri Madinda', 'Regina Zanzibar' na 'Mjini Mipango'.Waimbaji wanaotarajiwa kuburudisha onyesho hilo ni Rogert Hega 'Katapila', Ramadhani Masanja 'Banza Stone', Rama Pentagon, Bob Kisa, Athanas Muntanabe bila kusahau vionjo vya rapu za Saulo John Fergason.

Post a Comment

0 Comments