WAKONGWE WA MUZIKI WA KALE KUKESHA MKESHA WA SIKUKUU YA SABASA MZALENDO PUB

BAADA ya kusubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa muziki wa dansi nchini,hatimaye Usiku wa za Kale ni Dhahabu umefika ambapo moto wa aina yake utawashwa usuku wa leo jumatano Julai 6 ikiwa ni katika mkesha wa sikikuu ya Saba Saba ndani ya Mzalendo Pub Millennium Towers kijitonyama kuanzia saa mbili kamili usiku.Mkurugenzi wa Mac D Promotion waandaaji wa onyesho Anthony Stephen amesema kila kitu kimekamili baada ya wiki mbili za wanamuziki wakongwe nchini Kikumbi Mwanza Mpango King Kiki na kundi lake la La Capital na wakongwe wenzake Tshimanga Kalala Asossa na Kasongo Mpinda Cleyton kufanya mazoezi ya nguvu tayari kuzikonga nyoyo za mashabiki watakaofika Mzalendo Pub usiku wa leo.Anthony amesema usiku wa leo zitapigwa nyimbo zote kali ambazo wakongwe hawa wamepata kuziimba wakiwa na bendi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Fransisca,Huba,Seya,Angelou,Kibela acha chuki,Kitambaa cheupe,Nimepigwa ngwala na nyinginezo nyingi.Hili ni onyesho la kwanza kwa wanamuziki hawa kupiga pamoja katika jukwaa moja,hivyo amewataka mashabiki kuja kufuruhia mkesha wa Saba Saba na vitambaa vyeupe mkononi katika onyesho hilo lililodhaminiwa na Double View Hotel,Bandawe Freigth Tanga,DenFrance Hotel,Sk Bake Place,Screen Masters na Florida Executive Inn.Kutokana na maombi ya mashabiki wengi ambao wamekuwa na hamu kubwa ya kushuhudia wakongwe hawa wa muziki wakiimba pamoja jukwaani,Mac D Promotion imeweka kiingilio kuwa shilingi 5,000/= tu na ulinzi utakuwa niwa uhakika na burudani itatolewa bila kikomo.

Post a Comment

2 Comments

Anonymous said…
Khadija! tafadhali sana dear fanya kila uwezalo uhudhurie onesho hili itupe uhondo ktk blog hii ili sisi tulio mbali tuwe karibu na nyumbani.
Anonymous said…
Vipi umesha wasilikwenye kipupwe iringa? umejiandaaandaaje?