Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete akiwasha taa katika jengo la CCM Makao Makuu Lumumba ambapo ndipo sehemu ilipozaliwa TANU Julai 7 1954.Sherehe hizo zimefanyika usiku wa mkesha wa sikukuu ya sabasaba.
Hapa Mwenyekiti wa CCM akiwa katika Viwanja vya Mnazi mmoja katika sherehe za miaka 50 ya kuzaliwa kwa TANU.
Mama Salma Kikwete akijumuika na wanamuziki wa bendi ya Vijana Jazz
Mama Salma Kikwete alishindwa kujizuia kwani wakati burudani zikiendelea kutolewa nayeye alijiamua kujimwaya mwaya jukwaani wakati bendi ya Vijana Jazz wakitoa burudani.
Katibu Uenezi wa Chama Tawala Chama Cha Mapinduzi CCM , Nape Mnauye akipuliza Tarumbeta hapa ilikuwa nje ya Ofisi ya CCM Lumumba, huku akishuhudiwa na watu waliokuwepo katika viunga hivyo.
TID akiwa jukwaani pamoja na kikosi kazi chake kwa raha zao hapa akionyesha umahiri mbele ya kadamnasi iliyojitokeza kwenye sherehe hizo zilizofana.
Ni katika kunogesha burudani huku mzuka ukiwa umepanda huyu ni TID pamoja na bendi yake.
TID akiwa na bendi yake , vijana hawakuachwa nyuma walipewa nafasi ya kutoa burudani kama inavyoonekana.
Kijana mtanashati Khalid Mohammed TID, alitoa burudani akiwa na bendi yake katika sherehe hizo.
Waimbaji wa kike wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT), wakiwa wamejiegesha.
Vijana Jazz wakiwa jukwaani. Mbali ya bendi hiyo pia bendi ya The African Stars Twanga Ppepeta nao walitumbuiza mwanzo kabla ya bendi zingine kupanda pamoja na msanii Marow nayeye alitoa burudani. Bendi ya Vijana Jazz wakiwa jukwaani ambapo walitoa burudani iliyokonga nyoyo za mashabiki.
Makada wa Chama Cha Mapinduzi CCM hapa wakimlaki Mwenyekiti wa Chama hicho hayupo pichani Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akiwasili CCM Lumumba.
Baadhi ya watu waliojitokeza katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es Salaam kwenye sherehe hizo.
Katimu Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Nape Mosses Mnauye akikung'uta jukwaa la Bass akiwa na bendi ya Vijana Jazz.
Mwanamuziki wa bendi ya TOT , Abdul Misambano akiwa jukwaani katika mkesha wa sikukuu ya kumbukumbu ya kuzaliwa Chama Cha TANU.
Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni Mstaafu John Komba akiwa na kundi lake la Tanzania One Theatr (TOT).
Mtoto huyu alionekana kuvutiwa na kila mwanamuziki aliyepanda jukwaani na alikuwa akiimba na kucheza nyimbo zote hapa alikuwa akimtazama mwanamuziki TID, alikuwa akisimama pale mashairi yalipoonekana kumtachi na baadaye alikua akiendelea kucheza na kuimba katika viwanja hivyo vya Mnazi mmoja lakini hakuwa tayari kutaja jina lake ila picha alikubali kupigwa.
0 Comments