Social Icons

Tuesday, July 12, 2011

SERIKALI YAHUZUNISHWA KUKATWA UMEME U/TAIFA



Serikali imehuzunishwa sana na tukio la kukatwa umeme wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame kati ya vilabu vya Simba na Yanga ambapo umeme ulikatika ghafla kwenye Uwanja wa Taifa. Wizara inawaomba radhi wapenzi wa soka wa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kwa usumbufu uliojitokeza.
Tukio hilo ambalo siyo la kawaida halikutazamiwa. Tunapenda kuwaahidi wananchi, hususani wapenda michezo, kwamba tukio la aina hiyo halitatokea tena. Aidha, Serikali inawashukuru wananchi wote waliojitokeza uwanjani hapo kushuhudia mchezo wa jana kwa kuwa watulivu wakati wote wa tukio hilo hadi umeme uliporejeshwa. Kwa kutambua uzito wa suala hili, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeunda Kamati ya watu wanne (4) kuchunguza sababu zilizosababisha umeme kukatika na kukosekana uwanjani hapo. Kamati hiyo itaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Bi. Sihaba Nkinga. Wajumbe wengine ni Bw. Charles Bagenda, Mkuu wa Kitengo cha Umeme cha Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Bw. Mohamed Kiganja, Kaimu Katibu Mkuu, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Bi. Anna Chungu, Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Wizarani.

No comments:

 
 
Blogger Templates