MISS KINONDONI WAFUNDWA

Warembo wa shindano la Redds Miss Kinondoni 2011 wametakiwa kulinda heshima yao katika jamii kwa kufanya mambo mema yatakayotoa mwongozo kwa wanajamii hasa wanawake.
Wito huo ulitolewa jana na Meneja wa kinywaji cha Redds Victoria Kimaro wakati akizungumza na warembo waliofika katika kiwanda cha Tanzania Breweries Limited (TBL) Ilala.
Victoria alisema kuwa warembo wanaoshiriki shindano la Redds Kinondoni wanao wajibu wa kuwafundisha wanajamii masuala mbalimbali yahusuyo ukwimwi, Malaria na masuala mengine muhimu yanayoigusa jamii.
Victoria alisema kuwa warembo wanaweza kuifundisha na kuibadilisha jamii kuondokana na dhana potofu mbalimbali ambazo zinaathari katika jamii na kuiweka jamii katika mstari ulionyooka.
Aliwataka warembo hao kutambua kuwa ushupavu ndio njia pekee ikayowawezesha kufika mbali ikiwa pamoja na kufikia ndoto zao za baadae.
“Ni kwamba mtazamo wa Redds ni kuhusu suala la kujiamini, kujitambua na kuwa na maadili na ndio maana kupitia kinywaji hiki tumeamua kuwafikia akinadada kupitia kinywaji cha Redds kwa kudhamini masuala ya urembo” alisema Victoria.Warembo wa shindano hilo walipata nafasi ya kuzungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho ikiwa pamoja na kujionea shughuli mbalimbali za kiwandani hapo, shindano la Redds Miss Kinondoni linafanyika Jumamosi ijayo katika ukumbi wa Mlimani City.

Post a Comment

0 Comments