KIINGILIO CHA JUU MECHI YA TIMU YA VUJANA U-23 v NIGERIA NI SH.10,000



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIJuni 1, 2011



VIINGILIO U 23 v NIGERIA



Mechi ya kwanza ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati ya timu ya Taifa yaTanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23 dhidi ya Nigeria itafanyikaJumapili (Juni 5, 2011) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamilijioni.

Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 1,000 kwa viti vya kijani, bluu narangi ya chungwa (orange straight and curve), sh. 5,000 kwa VIP C na B na sh.10,000 kwa VIP A.

Tiketi zitaanza kuuzwa Ijumaa saa 2 asubuhi kwenye vituo vyaShule ya Sekondari Benjamini Mkapa, Bigbon Msimbazi (Kariakoo), Steers (Mtaa waOhio na Samora), Uwanja wa Uhuru, Ubungo OilCom na vituo vya mauzo vya PremierSports Betting.

Nigeria itawasili Juni 3 mwaka huu kama ilivyo kwa waamuzi wa mechi hiyo kutokaKenya na Kamishna kutoka Ethiopia.

Mwamuzi ni Sylvester Kirwa ambaye atasaidiwana Peter Kiereini, Aden Marwa na Davies Omweno wakati Kamishna ni SahiluGebremariam.

Pia TFF kupitia Kurugenzi ya Masoko imepiga marufuku wachuuzi wa viburudishokwenye mechi hiyo, isipokuwa kwa kampuni maalumu iliyopewa kazi hiyo.

Hivyovijana wote watakaofanya biashara bila kibali cha TFF watakamatwa.

Suala hilipia linawahusu wachuuzi wa jezi za timu ya Taifa uwanjani.

KALENDA YA MATUKIO TFF

imetoa kalenda yake ya matukio kwa mwaka 2011/2012 ambapo kipindi cha kwanzacha matayarisho ya msimu kinaanza Juni 1 hadi Agosti 13 mwaka huu.

Kipindi chakwanza cha uhamisho kinaanza Juni 1 hadi Julai 15 ambapo usajili wa kwanzautakuwa Juni 1 hadi Julai 20.

Kutangaza wachezaji wa kuachwa/kusitisha mikataba ni kuanzia Juni 1 hadi 21mwaka huu wakati kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya Julai 21-31mwaka huu.

Kipindi cha pili cha uhamisho kitaanza Novemba 1 hadi 20 mwaka huu wakatiusajili utaanza Novemba 1 hadi 30 mwaka huu.

Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacominatarajiwa kutoka Julai 20 mwaka huu. Ngao ya Hisani kwa ajili ya ufunguzi wamsimu kwa mikoa yote itachezwa Agosti 13 mwaka huu wakati mzunguko wa kwanza waLigi Kuu ya Vodacom utaanza Agosti 20 mwaka huu.

TFF tunawaomba wadau wote kuhakikisha wanapata kalenda hii ili waweze kupangashughuli na mipango yao kwa kuizingatia.

WACHEZAJI DAN MRWANDA NA ABDI KASSIM WAZUIWA VIETNAM

achezaji Danny Mrwanda na Abdi Kassim ni miongoni wa wachezaji saba wanaocheza mpira wakulipwa nje ya nchi walioitwa na kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen kwa ajili yamechi dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati itakayofanyika Juni 5 mwaka huu jijini Bangui.

Klabu yao ya Dong Tam Long ya Vietnam imekataa kuwaruhusu wachezaji hao kujiungana Stars kwa madai kuwa iko kwenye hali ngumu katika ligi yao.

Timu hiyoinashika nafasi ya mwisho kwenye ligi ya nchi hiyo inayoshirikisha timu 14,hivyo kudai kuwa wachezaji hao ni muhimu kwao kuwaokoa kutoka mkiani.

TFF tumepinga hatua hiyo kwa vile ni kinyume na Kanuni ya Hadhi na Uhamisho waWachezaji (Regulations of Status and Players Transfer), hivyo tutawasilishamalalamiko yetu kwa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

KOZI YA WAKUFUNZI WA WAAMUZI

Kozi ya Wakufunzi (Instructors) wa Waamuzi wa Mikoa imeanza leo (Juni Mosi)jijini Dar es Salaam ikishirikisha wakufunzi 16 kutoka mikoa mbalimbali yaTanzania Bara.

Wawezeshaji katika kozi hiyo itakayomalizika Juni 4 mwaka huu na inayofanyika Ofisi za TFF ni Hafidh Ally, Leslie Liunda, Joseph Mapunda, Riziki Majala naJuma Ali David.

Boniface Wambura

Ofisa Habari TFF

Post a Comment

0 Comments