TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIMei 17, 2011
KITUO CHA KUKUZA VIPAJI CHA TSA
Kituo cha kukuza vipaji cha Tanzania Soccer Academy (TSA) kinachoendeshwa kwaubia kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Kiliwoodkimesimamisha shughuli zake tangu mwaka jana. Kamati ya Utendaji katika kikao chake cha kwanza mwaka huu ilishafanya uamuzijuu ya uendeshaji wa kituo hicho na kutoa maelekezo kwa Sekretarieti ya TFF. Kwavile kituo hicho kilichokuwa kinachukua vijana wenye umri kuanzia miaka 17 hadi20 ni cha ubia kati ya TFF na Kiliwood uamuzi wowote juu ya mustakabali wake nilazima uhusishe pande hizo mbili. Kwa mantiki hiyo Sekretarieti kwa sasa inafanya mawasiliano na kampuni yaKiliwood ili pande hizo mbili zikutane na kuelezana juu ya uamuzi wa Kamati yaUtendaji ya TFF juu ya mustakabali wa kituo hicho. Wajibu wa TFF katika mkataba kati yake na Kiliwood juu ya uendeshaji wa kituohicho ni vitendea kazi (facilities) ambavyo ni hosteli na uwanja wa mazoezi.
KOZI YA WAKUFUNZI WA MAREFA TFF
kupitia Kurugenzi ya Ufundi imeandaa kozi ya wakufunzi wa marefa wa mikoaitakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Juni 1 hadi 4 mwaka huu. Kozi hiyo inatarajia kushirikisha wakufunzi wa marefa zaidi ya 20 kutoka mikoayote ya Tanzania Bara. Mara ya mwisho kozi hiyo ilifanyika nchini mwaka 2008. Wawezeshaji katika kozi hiyo ni Stanley Lugenge ambaye ni Mwenyekiti wa Kamatiya Waamuzi ya TFF, Leslie Liunda, Joseph Mapunda, Hafidh Ally na Juma Hamisi.
Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF
0 Comments