UONGOZI wa The African Stars Entertainment 'ASET' jana umetoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa wamemtimua msanii mkonge na mmmoja wa waasisi wa bendi hiyo Adolph Mbinga kutokana na kosa la kutotimiza wajibu wake katika bendi hiyo kama ilivyotarajiwa tangu aliporejea tena akundini mwishoni mwa mwaka jana.
Wakati huohuo 'ASET' ambao wanamiliki bendi ya Twanga Pepeta wameingia katika mchakato wa kumsaka mpiga gitaa mwingine atakayeziba pengo la Mbinga.
Baada ya kung'olewa Mbinga safu ya wapiga magitaa ya Twanga waliobaki ni pamoja na Miraji Shakashia 'Shaka Zulu', Jumanne Said Mkandu 'Jojo Jumanne', Godfrey Kanuti na Kado Hassan.
Mbinga hakuwa na mkataba na 'ASET' hivyo katika kipindi hicho alipokuwa kazini alikuwa kwenye kipindi cha uangalizi, hivyo hakuonyesha maendeleo yoyote alipokuwa katika bndi hadi tulipofikia uamuzi wa kumuondoa.Wakati akiwa katika bendi alilipwa stahili zake zote kutokana na makubaliano yetu .
ASET tutaendelea kuthamini mchango wa Adolph Mbinga ambaye alikuwa ni kati wanamuziki sita walioasisi bendi hii ikiwa ni pamoja na kuitunga nyuimbo zilizoipa jina bendi hii kabla ya kutimkia katika bendi ya Mchinga na kujaribu kuondoka na baadhi ya wanamuziki.
Martin Sospeter
Meneja wa Bendi.
0 Comments