Mti huu una kumbukumbu ya kutumika kwa kuwanyonga wahalifu katika enzi za utawala wa Mjerumani.
Hapa ni mgahawa ambapo nilipata kipooza koo yaani Juisi baridi pamoja na mlo.
Mechi ya michuano ya Kopa Coca Cola ikiendelea katika Uwanja wa Nyamagana leo jioni ambapo timu kati ya Sengerema na Magu.Chini wachezaji waliopiga picha ya pamoja ni timu ya u-17 Sengerema ambapo michuano hii iko katika hatua ya awali kuwania ubingwa wa Mkoa ambapo mabingwa watakwenda kucheza katika fainali Jijini Dar es Salaa. Timu zingine zinazoshiriki ni Nyamagana, Misungwi, Ilemela, Magu,Geita na Kwimba.
Kikosi cha timu Sengerema inayoundwa na vijana Chini ya umri wa miaka 17 kabla ya kujitupa uwanjani katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Nyamagana.
Lango kuu la kuingia kwenye Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.Kiota hiki zamani kilifahamika kwa jina la Rock Beach.
Kazi ni kazi.
Hili jiwe ambalo unaliona mdau linaonekana katika noti ya shilingi elfu moja litazame vizuri kisha angalia noti yako ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Meli moja MV Victoria ambayo ndiyo ilikuwa kubwa kuliko zote ikiwa imetia nanga. Boti tatu zikiwa majini katika Ziwa Victoria.
Ndege hawa wakifurahia maisha yao kandokando ya Ziwa.
Hapa ni duka la kuuza samaki lililopo kando ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza.
Ndege hawa wakifurahia maisha yao kandokando ya Ziwa.
Hapa ni duka la kuuza samaki lililopo kando ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza.
Wadau namshukuru mungu nimefika salama na tayari nimeanza mchakato wa kazi hapa Mwanza.Nami nikibarizi pembezoni mwa ziwa Victoria jioni ya leo nimevutiwa na mandhari ya Jiji la Mwanza kwa ujumla pamoja na hali ya hewa ni nzuri na isiyochosha.
0 Comments