RAGE ATANGAZA KLABU YA SIMBA KUWALETA BIRMINGHAM


Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Pia Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani leo.
Na Dina Ismail

Mabingwa wa kombe la Carling nchini Uingereza timu ya Birmingham Citywanatarajiwa kuja nchini mwezi Julai kwa ziara maalum ya kimichezoambapo watakipiga na vigogo wa soka nchini, timu za Simba na Yanga.

Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage alisema jana kuwa baadhi yayamaofisa wa juu wa timu hiyo akiwemo kocha msaidizi Andy Watson,pamoja na daktari wa timu Ian Mc Guinness wanatarajiwa kuwasili nchini Mei 9 kwa ajili ya kukagua Uwanja na hoteli.

Rage alisema ujumbe huo utakagua Uwanja wa Taifa utakaotumika pamojana hoteli ya Kilimanjaro Kempisk ili kuona kama vinakidhi vigezo vyatimu hiyo ambayo itaambatana na mashabiki wasiopungua 1000 ambaowatajilipia gharama za hoteli na uwanjani.

Alisema usiku wa Julai 7 Birmingham itakipiga na Simba kabla ya jioniya Julai 12 kukipiga na mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa2010/2011 Yanga.

“Tunafurahi kupata wasaa wa kuwa wenyeji wa timu kubwa kama hiyo, ujiowao huo utafungua mipaka ya kimataifa baina yetu na wao…tayaritumeshazungumza na watu wa Wizara ya Maliasili na utalii juu ya ujiohuo”, Alisema Rage.

Kwa upande mwingine Rage alisema mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama waklabu hiyo unatarajiwa kufanyika Mei 15 katika Bwalo la Maofisa wapolisi Oyesterbay jijini Dar es Salaam na kusema kuwa wanachamawatakaoruhusiwa kushiriki ni wale ambao watakuwa wamelia ada.

Alisema kila mwanachama anatakuiwa kulipa ada ya mwaka shilingi 12,000pamoja na ile ya uwanja shilingi 20,000 na kwamba malipo hayo yafanywekatika akaunti ya wanachama.Aidha, Rage lisema uongozi umtoa saa 48 kwa wapangaji wanaotakakuendelea kupanga katika jengo lao kuwasiliana na uongozi kinyume chahapo watakwenda kuomba kibali chama mahakama kwa ajili ya kuwaondoakwa nguvu.

Wakati huohuo, beki wa timu hiyo Kelvin Yondan amewasilisha barua yakuomba msahama kutokana na utovu wa nidhamu huku akiomba arudishwekundini.Wakati mshambuliaji Mussa Mgosi ambaye naye aliadhibiwakutokana na kukiuka mkataba kwa kuzungumza sana na vyombo vya habariakitakiwa kusoma upya mkataba wake na kutoa maelezo.

Post a Comment

0 Comments