AL ANISA FATMA KIDOGO AZIKWA DAR ES SALAAM LEO





Aliyekuwa Mwimbaji mkongwe wa kundi la Tanzania One Theatre ‘TOT Taarab’, FatmaAlly ‘Dogodogo’ (49), amezikwa saa 7:00 kwenye makaburi yaMwananyamala kwa Kopa jijini Dar es Salaam.


Dogodogo, alifariki jana majira ya saa 8:00 mchana kwenye Hospitali yaMwananyamala jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na kansa ya kizazi.


Wakati wa uhai wake, Dogodogo alijiunga na TOT, Agosti 1993,alitamba vilivyo na vibao kadha wa kadha vikali kama vile ‘Tamtam’,‘Upinde’, ‘Asojijiua’, ‘Hujawa Mcheza’ na ‘Utaniona Hivi Hivi’.Aidha, aliweza kumudu kukonga nyoyo za mashabiki pamoja na wapenzi wataarab na kutokea kuwa kivutio kwa wengi, kutokana na uimbaji wake,miondoko pamoja na uchezaji wa aina yake.Akizungumza baada ya mazishi hayo leo, Mkurugenzi wa TOT, Kapteni mstaafu JohnKomba, alisema kundi lake limesimamisha shughuli zote za burudani kwa juma moja, ambapo watakuwa wanaomboleza.


Marehemu Dogodogo, ameacha mtoto mmoja, pamoja na wajukuu watatu:Sharifa, Fatma na Nasma.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Amin.

Post a Comment

0 Comments