Mabingwa wa Afrika katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa, Tout Puissant TP MAZEMBE ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo RDC, leo imewalazimisha kufunga virago na kuwaondoa Mabingwa wa Tanzania , Simba katika mashindano hayo ya Afrika baada ya kukubali kichapo cha magoli 3-2 Simba katika mchezo wa awamu ya pili uliochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa .Katika mchezo huo TP Mazembe waliweza kutumia vizuri dakika 20 za awali , kwani mshambuliaji wa timu hiyo Given Singuluma alikosa magoli kadhaa katika dakika hizo , huku Simba nayo ikikosa magoli kadhaa katika dakika hizo kupitia kwa washambulaiji wake kama Mussa Hassan Mgossi na Mbwana Samata .Goli la kwanza la timu ya TP Mazembe lilifungwa na Given Singuluma katika dakika ya 16. Hadi kipindi cha kwanza kinaisha TP Mazembe ilikuwa ikiongoza kwa goli moja . Katika kipindi cha pili kilianza ambapo dakika ya 58 ya mchezo mchezaji wa Simba , Shija Mkina aliipachikia goli la kusawazisha timu yake.Aidha ilipofika dakika ya 63 ya mchezo, Alain Kaluyitika aliipachikia goli la pili timu yake ya TP Mazembe. Katika dakika ya 65 ya mchezo, Simba ikapachika ilisawazisha na kuwa 2-2 goli lilopatikanba kwa kupitia mchezaji wake chipukizi Mbwana Samata, goli ambalo halikudumu kwa muda mrefu kwani Alain Kaliyitika alipachika goli la tatu kwa timu yake. Simba imetolewa kwa jumla ya magoli 6-3 kwani katika mchezo wa awali uliofanyika DRC dhidi timu ya TP Mazembe, wekundu nhao wa Msimbazi walichapwa 3-1.
MAWAZIRI WATATU WAJADILI MAENDELEO YA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI
-
*Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza kuhusu
uendelezaji wa sekta ya madini ili kukuza uchumi wa nchi, wakati akiongoza
kika...
6 minutes ago
0 Comments